The chat will start when you send the first message.
1Heri wote wamchao Mwenyezi-Mungu,
wanaoishi kufuatana na amri zake.
2Utapata matunda ya jasho lako,
utafurahi na kupata fanaka.
3Mkeo atakuwa kama mzabibu wa matunda mengi nyumbani mwako;
watoto wako kama chipukizi za mzeituni kuzunguka meza yako.
4Naam, ndivyo atakavyobarikiwa
mtu amchaye Mwenyezi-Mungu.
5Mwenyezi-Mungu akubariki kutoka Siyoni!
Uione fanaka ya Yerusalemu, siku zote za maisha yako.
6Uishi na hata uwaone wajukuu zako!
Amani iwe na Israeli!