The chat will start when you send the first message.
1Toka upeo wa unyonge wangu,
nakulilia, ee Mwenyezi-Mungu.
2Ee Bwana, sikia sauti yangu,
uitegee sikio sauti ya ombi langu.
3Kama, ee Mwenyezi-Mungu ungekumbuka maovu yetu
nani, ee Bwana, angeweza kusalimika?
4Lakini kwako twapata msamaha,
ili sisi tukuheshimu.
5Namtumainia Mwenyezi-Mungu kwa moyo wangu wote;
nina imani sana na neno lake.
6Ninamtumainia Mwenyezi-Mungu
kuliko walinzi wanavyongojea pambazuko;
kuliko walinzi wanavyongojea kuche asubuhi.
7Ee Israeli, umtumainie Mwenyezi-Mungu,
maana kwake Mwenyezi-Mungu kuna fadhili,
kwake kuna nguvu kubwa ya kutukomboa.
8Yeye atawakomboa watu wa Israeli[#Taz Mat 1:21; Tito 2:14]
kutoka katika maovu yao yote.