Esta G 10

Esta G 10

Ukuu wa Ahasuero na Mordekai

1Mfalme Ahasuero alitoza kodi watu wa bara na pwani.

2Matendo yake yote makuu na ya ajabu, pamoja na simulizi kamili kuhusu jinsi alivyompandisha cheo Mordekai na kumtunukia heshima kuu, yote yameandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Media na Persia.[#10:2 Kitabu cha namna hiyo hakijulikani au hakikuhifadhiwa.]

3Mordekai, Myahudi, alikuwa wa kwanza chini ya mfalme Ahasuero katika madaraka. Alipendwa na kuheshimiwa na Wayahudi, maana aliwafanyia mema watu wake na kuwatakia amani wazawa wao wote.

Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993 The Bible Society of Kenya 1993
Published by: Bible Society of Tanzania