The chat will start when you send the first message.
1Naye akaniambia, “Wewe mtu! Simama wima. Nataka kuongea nawe.”[#2:1 Kiebrania “ben’adam”: Jina linalotumiwa mara nyingi Mungu anapomwita au kumtaka Ezekieli kufanya kitu fulani. Msemo huo wataka kukumbusha kwamba mtu ni kiumbe (sio Mungu) na ana hali yake hafifu na hufa; kwa hiyo huhitaji nguvu ya Mungu kumwongoza.]
2Alipokuwa akiongea nami, roho ya Mungu ikaniingia na kunisimamisha wima. Ndipo nikamsikia
3akiniambia, “Wewe mtu nakutuma kwa Waisraeli, taifa la waasi ambao wameniasi. Wameendelea kunikosea mimi hadi leo kama walivyokuwa wazee wao.[#2:3 Makala ya Kiebrania: “mataifa”.]
4Watu hao ni wafidhuli na wajeuri. Nakutuma kwao, nawe utawaambia kwamba mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi na hivi.
5Wakisikia au wasiposikia, maana wao ni watu waasi, walau watatambua kwamba nabii amekuwapo miongoni mwao.
6Lakini, ewe mtu usiwaogope hao wala maneno yao. Hata kama mbigili na miiba vinakuzunguka, au unaketi juu ya nge, usiogope maneno yao wala usitishwe na nyuso zao, kwani hao ni watu waasi.
7Wewe utawaambia maneno yangu, hata kama watasikia au hawatasikia, maana wao ni watu waasi.
8“Lakini ewe mtu, sikiliza ninayokuambia, wala usiwe mwasi kama watu hao. Fumbua kinywa chako, ule ninachokupa.”
9Nilipotazama, niliona nimenyoshewa mkono, na kumbe ulikuwa na kitabu kilichoandikwa.[#2:9 Neno linalotumika katika Kiebrania linaashiria umbo la vitabu vya nyakati hizo, yaani karatasi (papiri) au ngozi nyembamba zilizoviringwa na kutumiwa kuandikia. Pengine kwa usahihi zaidi ni “msokoto wa kuandikia”.]
10Basi akakifungua mbele yangu, nacho kilikuwa kimeandikwa mbele na nyuma maneno ya maombolezo, vilio na laana.[#2:10 Yamkini nabii anamaanisha kwamba maneno anayotakiwa kuwaambia watu ni mengi hivyo kwamba hamna nafasi ya kuyaandika yote kitabuni.]