The chat will start when you send the first message.
1Kisha Roho alimwongoza Yesu mpaka jangwani ili ajaribiwe na Ibilisi.[#4:1 Au “ashawishiwe”. Kukaa kwa Yesu kule jangwani kwa siku arubaini bila kula na majaribu anayopata kunakumbusha mambo yaliyowasibu Waisraeli kule jangwani walipotoka Misri. Waisraeli walishindwa katika majaribu yale waliyopata, lakini Yesu anabaki imara na mwaminifu kwa jukumu alilopewa. Rejea Ebr 2:18; 4:15.; #4:1 (Kigiriki: “Diabolos”) ni mojawapo ya majina ya Shetani, na jina hilo lina maana ya “Mpinzani”.]
2Akafunga siku arubaini mchana na usiku, na mwishowe akaona njaa.[#4:2 Tarakimu “arubaini” inakumbusha hapa historia ya Mose na Waisraeli (Kut 24:18; 34:28; Hes 14:33-34; 32:13) na Elia (1Fal 19:8).]
3Basi, mshawishi akamjia, akamwambia, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.”[#4:3 Rejea Mat 27:40. Yesu alipobatizwa alitangazwa rasmi kuwa Mwana wa Mungu (Mat 3:17) jina la sifa ambalo linamtaja Masiha. Kulingana na mapokeo ya Kiyahudi, wakati Masiha atakapokuja miujiza ya wakati wa Mose itafanyika tena. Ama kweli Ibilisi anamshauri Yesu afanye muujiza unaofanana na ule wa mana kule jangwani (Kut 16; tazama pia Yoh 6:30-36) ila hapa kwa faida yake Yesu mwenyewe]
4Yesu akamjibu, “Imeandikwa:
‘Mtu haishi kwa mkate tu,
ila kwa kila neno asemalo Mungu.’”
5Kisha Ibilisi akamchukua mpaka Yerusalemu, mji mtakatifu, akamweka juu ya mnara wa hekalu,
6akamwambia, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini; maana imeandikwa:
‘Mungu atawaamuru malaika wake kwa ajili yako;
watakuchukua mikononi mwao,
usije ukajikwaa kwenye jiwe.’”
7Yesu akamwambia, “Imeandikwa pia:
‘Usimjaribu Bwana, Mungu wako.’”
8Kisha Ibilisi akamchukua mpaka juu ya mlima mrefu, akamwonesha falme zote za ulimwengu na fahari zake,
9akamwambia, “Hivi vyote nitakupa kama ukipiga magoti na kuniabudu.”
10Hapo, Yesu akamwambia, “Nenda zako Shetani! Imeandikwa:[#4:10 Jina ambalo lina maana ya “Mshtaki” au hata “Mpinzani” na ambalo linatumiwa pia kumtaja Ibilisi.]
‘Utamwabudu Bwana Mungu wako
na kumtumikia yeye peke yake.’”
11Basi, Ibilisi akamwacha, na malaika wakaja, wakamhudumia.
12Yesu aliposikia kwamba Yohane ametiwa gerezani alikwenda Galilaya.[#4:12 Luka 3:19-20. Herode Antipa, mtawala wa Galilaya na Perea, ndiye aliyemtia Yohane gerezani. Taz Mat 14:3 na Marko 6:17-18.]
13Aliondoka Nazareti, akaenda Kafarnaumu, mji ulio kando ya bahari ya Genesareti, mpakani mwa wilaya za Zebuluni na Naftali, akakaa huko.[#4:13 Haya yalikuwa makabila mawili ya kale, kusini mwa Israeli. Wakati huo wakazi wake hawakuwa Wayahudi. Maeneo hayo ambayo wakati uliopita yaliathiriwa sana na vita sasa yatapata tena baraka za Mungu. Taz Mat 1:22.]
14Ndivyo lilivyotimia lile neno lililosemwa kwa njia ya nabii Isaya:
15“Nchi ya Zebuluni na nchi ya Naftali,
kuelekea baharini ng'ambo ya mto Yordani,
Galilaya, nchi ya watu wa mataifa!
16Watu waliokaa gizani
wameona mwanga mkubwa.
Nao walioishi katika nchi ya giza na kivuli cha kifo,
mwanga umewaangazia!”
17Tangu wakati huo Yesu alianza kuhubiri akisema, “Tubuni, maana ufalme wa mbinguni umekariia!”
18Yesu alipokuwa anatembea kando ya ziwa Galilaya, aliwaona ndugu wawili wavuvi; Simoni (aitwaye Petro) na Andrea, ndugu yake; walikuwa wakivua samaki kwa nyavu ziwani.[#4:18 Anaitwa pia “Petro”; taz Mat 16:18.]
19Basi, akawaambia, “Nifuateni, nami nitawafanya nyinyi wavuvi wa watu.”[#4:19 Neno Yesu alilotumia mara kwa mara alipoita watu ili wawe wanafunzi wake. Taz pia 9:9; Marko 1:17; 2:14; Marko 1:20; Luka 5:1-11.]
20Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata.[#4:20 Siyo tu kuandamana naye na kusikiliza mafundisho yake, bali aghalabu kumtii, kumstahi na kushirikiana naye kikamilifu. Taz pia 9:9; Marko 1:18; 2:14; Luka 5:28.]
21Alipokwenda mbele kidogo, aliwaona ndugu wengine wawili: Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo. Hao walikuwa ndani ya mashua pamoja na baba yao Zebedayo, wakitengeneza nyavu zao. Basi, Yesu akawaita,
22nao mara wakaiacha mashua pamoja na baba yao, wakamfuata.
23Yesu alikuwa anakwenda kila mahali wilayani Galilaya, akifundisha katika masunagogi na kuhubiri Habari Njema juu ya ufalme wa Mungu. Aliponya kila namna ya maradhi na magonjwa waliyokuwa nayo watu.[#4:23 Nyumba ambamo Wayahudi walikutana siku za Sabato kwa ibada na masomo au mafundisho ya Maandiko Matakatifu. Wakati wa kukutana huko kiongozi wa kikao aliweza kumwalika yeyote aliyekuwako kueleza au kufafanua Maandiko hayo Matakatifu (rejea Luka 4:16-21; Mate 13:14-15).]
24Habari zake zikaenea pande zote za Siria. Wagonjwa wote wenye maradhi ya kila namna na wale waliosumbuliwa na kila namna ya taabu: waliopagawa na pepo, wenye kifafa na watu waliokuwa wamelemaa, walipelekwa kwake; naye akawaponya wote.
25Makundi mengi ya watu kutoka Galilaya, Dekapoli, Yerusalemu, Yudea na ng'ambo ya mto Yordani, yalimfuata.[#4:25 Jina ambalo lilikuwa na maana ya “Miji kumi” tisa kati ya hiyo ilikuwa upande wa mashariki mwa Mto Yordani.]