Zaburi 133

Zaburi 133

Uzuri wa umoja kati ya watu

1Ni jambo zuri na la kupendeza sana

ndugu kuishi pamoja kwa umoja.

2Ni kama mafuta mazuri yatiririkayo kichwani,[#133:2 Mafuta yalitumiwa kumweka wakfu kuhani mkuu. Taz 2:2 maelezo. Si rahisi kuelewa matumizi ya kitendo hicho cha kumpaka mafuta Aroni. Wengi wanafikiri kwamba kama vile hayo mafuta yalivyoenea ndivyo ulivyo uhusiano wa kudumu kati ya ndugu. Lakini hakuna maelezo ya kutosheleza kabisa juu ya mfano huu.]

mpaka kwenye ndevu zake Aroni,

mpaka upindoni mwa vazi lake shingoni.

3Ni kama umande wa mlima Hermoni,

uangukao juu ya vilima vya Siyoni!

Huko Mwenyezi-Mungu ameahidi kuwabariki watu wake,

kuwapa uhai usio na mwisho.

Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993 The Bible Society of Kenya 1993
Published by: Bible Society of Tanzania