Kutoka 6

Kutoka 6

1Kisha Bwana akamwambia Musa, “Sasa utaona kitu nitakachomfanyia Farao: Kwa sababu ya mkono wangu wenye nguvu atawaachia watu waende; kwa sababu ya mkono wangu wenye nguvu atawafukuza waondoke nchini mwake.”

2Pia Mungu akamwambia Musa, “Mimi ndimi Bwana .

3Nilimtokea Abrahamu, na Isaka, na Yakobo kama Mungu Mwenyezi, ingawa kwa Jina langu, Yehova , sikujitambulisha kwao.[#6:3 Kiebrania El-Shaddai (yaani Mungu Mwenye utoshelevu wote).]

4Pia niliweka agano langu nao kuwapa nchi ya Kanaani, ambako waliishi kama wageni.

5Zaidi ya hayo, nimesikia kilio cha huzuni cha Waisraeli ambao Wamisri wamewatia utumwani, nami nimelikumbuka agano langu.

6“Kwa hiyo, waambie Waisraeli: ‘Mimi ndimi Bwana , nami nitawatoa katika nira ya Wamisri. Nitawaweka huru mtoke kuwa watumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyooshwa pamoja na matendo makuu ya hukumu.

7Nitawachukua ninyi kuwa watu wangu mwenyewe, nami nitakuwa Mungu wenu. Ndipo mtajua kuwa mimi ndimi Bwana Mungu wenu, niliyewatoa chini ya nira ya Wamisri.

8Nami nitawaleta hadi nchi niliyoapa kwa mkono ulioinuliwa kumpa Abrahamu, Isaka na Yakobo. Nitawapa iwe milki yenu. Mimi ndimi Bwana .’ ”

9Musa akawaarifu Waisraeli jambo hili, lakini hawakumsikiliza kwa sababu ya kuvunjika moyo na kazi yao ngumu.

10Ndipo Bwana akamwambia Musa,

11“Nenda, mwambie Farao mfalme wa Misri awaachie Waisraeli waondoke nchini mwake.”

12Lakini Musa akamwambia Bwana , “Ikiwa Waisraeli hawatanisikiliza, kwa nini yeye Farao anisikilize mimi, ambaye huzungumza kwa kigugumizi?”

Orodha ya jamaa ya Musa na Haruni

13Ndipo Bwana akanena na Musa na Haruni kuhusu Waisraeli na Farao mfalme wa Misri, naye akawaamuru wawatoe Waisraeli kutoka Misri.

Wana wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa kiume wa Israeli walikuwa:

15Wana wa Simeoni walikuwa:

16Haya ndiyo majina ya wana wa Lawi, kulingana na orodha zao:

20Amramu akamwoa Yokebedi, shangazi yake, aliyemzalia Haruni na Musa.

21Wana wa Ishari walikuwa:

22Wana wa Uzieli walikuwa:

23Haruni akamwoa Elisheba binti Aminadabu, ndugu yake Nashoni, naye akamzalia Nadabu na Abihu, Eleazari na Ithamari.

24Wana wa Kora walikuwa:

25Eleazari mwana wa Haruni akamwoa mmoja wa binti za Putieli, naye akamzalia Finehasi.

26Hawa walikuwa Haruni na Musa, wale wale ambao Bwana aliwaambia, “Watoeni Waisraeli katika nchi ya Misri kwa vikosi vyao.”

27Hao ndio waliozungumza na Farao, mfalme wa Misri kuhusu kuwatoa Waisraeli Misri. Ilikuwa ni huyo Musa na huyo Haruni.

Haruni kuzungumza badala ya Musa

28Bwana aliponena na Musa huko Misri,

29akamwambia, “Mimi ndimi Bwana . Mwambie Farao mfalme wa Misri kila kitu nikuambiacho.”

30Lakini Musa akamwambia Bwana , “Kwa kuwa mimi huzungumza kwa kigugumizi, Farao atanisikiliza mimi?”

Neno: Biblia Takatifu™ Neno™ Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 na Biblica, Inc. Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote. Kiswahili Contemporary Version™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc. Used with permission. All rights reserved worldwide.
Published by: Biblica, Inc.