The chat will start when you send the first message.
1Katika siku ile utasema:
“Nitakusifu wewe, Ee Bwana .
Ingawa ulinikasirikia,
hasira yako imegeukia mbali
nawe umenifariji.
2Hakika Mungu ni wokovu wangu;
nitamtumaini wala sitaogopa.
Bwana , Bwana , ni nguvu zangu na wimbo wangu;
amekuwa wokovu wangu.”
3Kwa furaha mtachota maji
kutoka visima vya wokovu.
4Katika siku hiyo mtasema:
“Mshukuruni Bwana , mliitie jina lake;
julisheni miongoni mwa mataifa yale aliyoyafanya,
tangazeni kuwa jina lake limetukuka.
5Mwimbieni Bwana , kwa kuwa ametenda mambo makuu,
hili na lijulikane duniani kote.
6Pazeni sauti mwimbe kwa furaha, watu wa Sayuni,
kwa maana mkuu ni yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli miongoni mwenu.”