The chat will start when you send the first message.
1Israeli alipotoka Misri,
nyumba ya Yakobo kutoka kwa watu wa lugha ngeni,
2Yuda alifanywa makao matakatifu ya Mungu,
Israeli akawa milki yake.
3Bahari ilitazama ikakimbia,
Yordani ulirudi nyuma,
4milima ilirukaruka kama kondoo dume,
vilima kama wana-kondoo.
5Ee bahari, ni nini kilichokufanya ukakimbia,
nawe, ee Yordani, ukarudi nyuma,
6enyi milima mkarukaruka kama kondoo dume,
enyi vilima, kama wana-kondoo?
7Ee dunia, tetemeka mbele za Bwana,
mbele za Mungu wa Yakobo,
8aliyegeuza mwamba kuwa dimbwi la maji,
mwamba mgumu kuwa chemchemi za maji.