The chat will start when you send the first message.
1Tazama jinsi ilivyo vyema na kupendeza
ndugu wanapoishi pamoja katika umoja!
2Ni kama mafuta ya thamani yaliyomiminwa kichwani,
yakitiririka kwenye ndevu,
yakitiririka kwenye ndevu za Haruni,
hadi kwenye upindo wa mavazi yake.
3Ni kama umande wa Hermoni
ukianguka juu ya Mlima Sayuni.
Kwa maana huko ndiko Mwenyezi Mungu alikoamuru baraka yake,
naam, uzima hata milele.