Zaburi 150

Zaburi 150

Zaburi 150

Msifuni Mwenyezi Mungu kwa ukuu wake

1Msifuni Mwenyezi Mungu.[#150:1 kwa Kiebrania ni Hallelu Yah ; pia 150:6.]

Msifuni Mungu katika patakatifu pake,

msifuni katika mbingu zake kuu.

2Msifuni kwa matendo yake makuu,

msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.

3Msifuni kwa mvumo wa tarumbeta,

msifuni kwa kinubi na zeze,

4msifuni kwa matari na kucheza,

msifuni kwa kinanda cha nyuzi na filimbi,

5msifuni kwa matoazi yaliayo,

msifuni kwa matoazi yavumayo sana.

6Kila chenye pumzi na kimsifu Mwenyezi Mungu.

Msifuni Mwenyezi Mungu!

Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote. Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc. Used with permission. All rights reserved worldwide.
Published by: Biblica, Inc.