The chat will start when you send the first message.
1Bwana anatawala,
mataifa na yatetemeke;
anakalia kiti cha enzi katikati ya makerubi,
dunia na itikisike.
2Bwana ni mkuu katika Sayuni;
ametukuzwa juu ya mataifa yote.
3Wanalisifu jina lako ambalo ni kuu na la kuogopwa:
yeye ni mtakatifu!
4Mfalme ni mwenye nguvu na hupenda haki,
wewe umethibitisha adili;
katika Yakobo umefanya
yaliyo haki na sawa.
5Mtukuzeni Bwana Mungu wetu,
na mkaabudu katika mahali pa kuwekea miguu yake;
yeye ni mtakatifu.
6Musa na Haruni walikuwa miongoni mwa makuhani wake,
Samweli alikuwa miongoni mwa walioliitia jina lake;
walimwita Bwana ,
naye aliwajibu.
7Alizungumza nao kutoka nguzo ya wingu;
walizishika sheria zake na amri alizowapa.
8Ee Bwana , wetu,
ndiwe uliyewajibu,
kwa Israeli ulikuwa Mungu mwenye kusamehe,
ingawa uliadhibu matendo yao mabaya.
9Mtukuzeni Bwana Mungu wetu,
mwabuduni kwenye mlima wake mtakatifu,
kwa maana Bwana Mungu wetu ni mtakatifu.