The chat will start when you send the first message.
1Napenda kumtambulisha kwenu dada yetu Foibe, mtumishi katika kanisa la Kenkrea.
2Naomba mpokeeni katika Bwana ipasavyo watakatifu na kumpa msaada wowote atakaohitaji kutoka kwenu, kwa maana yeye amekuwa msaada kwa watu wengi, mimi nikiwa miongoni mwao.
3Wasalimuni Prisila na Akila, watumishi wenzangu katika Kristo Yesu.[#16:3 kwa Kiyunani ni Priska]
4Wao walihatarisha maisha yao kwa ajili yangu; wala si mimi tu ninayewashukuru bali pia makanisa yote ya watu wa Mataifa.
5Lisalimuni pia kanisa linalokutana nyumbani mwao.
Msalimuni rafiki yangu mpendwa Epaineto, aliyekuwa mtu wa kwanza kumwamini Kristo huko jimbo la Asia.
6Msalimuni Mariamu, aliyefanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu.
7Wasalimuni Androniko na Yunia, jamaa zangu ambao wamekuwa gerezani pamoja nami. Wao ni maarufu miongoni mwa mitume, nao walikuwa katika Kristo kabla yangu.
8Msalimuni Ampliato, yeye nimpendaye katika Bwana.
9Msalimuni Urbano, mtendakazi mwenzetu katika Kristo, pamoja na rafiki yangu mpendwa Stakisi.
10Msalimuni Apele aliyejaribiwa na akaithibitisha imani yake katika Kristo.
Wasalimuni wote walio nyumbani mwa Aristobulo.
11Msalimuni ndugu yangu Herodioni.
Wasalimuni wote walio nyumbani mwa Narkiso walio katika Bwana.
12Wasalimuni Trifaina na Trifosa, wale wanawake wanaofanya kazi kwa bidii katika Bwana.
Msalimuni rafiki yangu mpendwa Persisi, mwanamke mwingine aliyefanya kazi kwa bidii katika Bwana.
13Msalimuni Rufo, mteule katika Bwana, pamoja na mama yake, ambaye amekuwa mama kwangu pia.
14Wasalimuni Asinkrito, Flegoni, Herme, Patroba, Herma na ndugu wote walio pamoja nao.
15Wasalimuni Filologo, Yulia, Nerea na dada yake, na Olimpa na watakatifu wote walio pamoja nao.
16Salimianeni kwa busu takatifu.
Makanisa yote ya Kristo yanawasalimu.
17Ndugu zangu, nawasihi mjihadhari na kujiepusha na wale watu waletao matengano na kuweka vikwazo mbele yenu dhidi ya mafundisho mliyojifunza.
18Kwa maana watu kama hao hawamtumikii Bwana wetu Kristo, bali wanatumikia tamaa zao wenyewe. Kwa kutumia maneno laini na ya kubembeleza, hupotosha mioyo ya watu wajinga.
19Kila mtu amesikia kuhusu utii wenu, nami nimejawa na furaha tele kwa ajili yenu. Lakini nataka mwe na hekima katika mambo mema na bila hatia katika mambo maovu.
20Mungu wa amani atamponda Shetani chini ya miguu yenu upesi.
Neema ya Bwana wetu Yesu iwe nanyi. Amen.
21Timotheo, mtendakazi mwenzangu anawasalimu. Vivyo hivyo Lukio, Yasoni, na Sosipatro, ndugu zangu.
22Mimi, Tertio, niliye mwandishi wa waraka huu, nawasalimu katika Bwana.
23Gayo, ambaye ni mwenyeji wangu na wa kanisa lote, anawasalimu.
Erasto, mweka hazina wa mji huu, pamoja na Kwarto ndugu yetu pia wanawasalimu.
[
24Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nanyi nyote. Amen.][#16:24 Maandiko mengine ya kale hayana maneno haya.]
25Sasa atukuzwe yeye awezaye kuwafanya imara kwa Injili yangu na kuhubiriwa kwa Yesu Kristo, kutokana na kufunuliwa siri zilizofichika tangu zamani za kale.
26Lakini sasa siri hiyo imefunuliwa na kujulikana kupitia maandiko ya kinabii kutokana na amri ya Mungu wa milele, ili mataifa yote yaweze kumwamini na kumtii:
27ndiye Mungu, aliye pekee mwenye hekima, ambaye kupitia kwa Yesu Kristo utukufu ni wake milele na milele! Amen.