The chat will start when you send the first message.
1Ni wengi waliokosa kwa ajili ya faida, naye atafutaye kizidisha utajiri atageuzia upande jicho lake.
2Kigingi kitashika kati ya miungo ya mawe, na dhambi itajipenyeza kati ya kununua na kuuza.
3Basi mtu asipokaza kumcha BWANA kwa bidii, nyumba yake itaangamizwa upesi.
4Kutikisa chekecheke, itabakishiwa;
Vile vile ila za mtu katika kujadili.
5Tanuri hujaribu vyombo vya mfinyanzi;
Vile vile jaribio la mtu ni kujadili.
6Matunda ya mti huonesha ulimaji wake;[#Mt 7:14; 12:33; Lk 6:44]
Vile vile kujadili mawazo ya moyoni.
7Usimsifu mtu usijemsikia anajadili;
Hakika hilo ni jaribio la wanadamu.
8Ukiifuata haki, hakika utaipata,
Na kujivika nayo kama kwa joho bora.
9Ndege hufanya kikao na ndege,
Na kweli itawarudia waifanyao.
10Simba huyaotea mawindo yake,
Na dhambi wao wafanyao uovu.
11Maongezi ya mtaalamu ni hekima siku zote,
Bali mpumbavu hubadilibadili kama mwezi.
12Katikati ya wajinga uiangalie nafasi yako,
Bali ukae daima pamoja na wazingativu.
13Mazungumzo ya wapumbavu ni machukizo,
na kucheka kwao ni tamaa mbaya ya dhambi.
14Matusi ya msafiri husimamisha nywele,
Na magomvi yao ni sababu ya kuziba masikio.
15Ugomvi wa wenye kiburi ni kumwaga damu,
Na matukano yao ni vigumu kuyasikia.
16Mwenye kufunua siri huivunja imani,[#Mit 20:19; 25:9]
Wala hatapata rafiki wa nafsi yake.
17Umpende rafiki yako, na uwe mwaminifu kwake; lakini ukizifunua siri zake, usifuate nyuma yake;
18kwa maana kama mtu kumharibu adui yake, wewe umeuharibu urafiki wa jirani yako.
19Kama ndege uliyemwachilia mkononi mwako, umemwacha jirani yako, wala humpati tena;
20usimfuate, amekwenda zake mbali, ameokoka kama paa mtegoni.
21Mradi jeraha itakuja kufungwa, hata baada ya mashutumu kuna mapatano; bali mwenye kufunua siri hana tumaini.
22Mwenye kung'ong'a huwaza maovu,
Nawe amjuaye atajitenga naye.
23Ukiwa umekuwapo, atasema ya kupendeza, na kuyastahi maneno yako; ila hatimaye atakipotoa kinywa chake, na kuyatatiza yale maneno yako.
24Mambo mengi nimeyachukia, lakini hakuna mfano wa huyo; naye BWANA mwenyewe atamchukia.
25Atupaye jiwe juu hulitupa juu ya kichwa chake mwenyewe; na kwa pigo la hila waweza kujitia jeraha.
26Achimbaye shimo atalitumbukia; na mwenye kutega mtego atanaswa nao.
27Afanyaye maovu yatamrudia juu yake mwenyewe, asijue yamemjia kutoka wapi.
28Mzaha na shutumu hutoka kwa mwenye kutakabari, kwa hiyo kisasi kitamwotea kama simba.
29Wanaosimanga kuona anguko la mwenye adili watanaswa katika shabuka; kwa maumivu yao watadhoofu kabla ya kufa kwao.
30Hasira na ghadhabu, haya pia ni machukizo, na aliye mwenye dhambi yatampata.