The chat will start when you send the first message.
1Nao wana wa Isakari: Tola na Pua na Yasubu na Simuroni, ni watu wanne.[#1 Mose 46:13; 4 Mose 26:23-24.]
2Nao wana wa Tola: Uzi na Refaya na Yerieli na Yamai na Ibusamu na Samweli, hawa walikuwa vichwa vyao vya milango ya baba zao; wao wa Tola walikuwa mafundi wa vita wenye nguvu katika vizazi vyao, hesabu yao katika siku za Dawidi ilikuwa watu 22600.
3Nao wana wa Uzi: Iziraya, nao wana wa Iziraya: Mikaeli na Obadia na Yoeli na Isia, wote pamoja ni wakuu watano.
4Tena vizazi vya kwao vya milango ya baba zao vilikuwa vyenye vikosi vikubwa vya wapiga vita, watu 36000, kwani walikuwa wenye wanawake na watoto wengi.
5Nao ndugu zao wa koo zote za Isakari walikuwa mafundi wa vita wenye nguvu, walioandikwa katika kitabu cha udugu, wote pamoja walikuwa watu 87000.
6Wa Benyamini: Bela na Bekeri na Yediaeli, watu watatu.[#1 Mose 46:21; 1 Mambo 8:1-2.]
7Nao wana wa Bela: Esiboni na Uzi na Uzieli na Yerimoti na Iri, vichwa vitano vya milango ya baba zao, nao walikuwa mafundi wa vita wenye nguvu nyingi; walioandikwa katika kitabu cha udugu walikuwa watu 22034.
8Wana wa Bekeri: Zemira na Yoasi na Eliezeri na Eliyoenai na Omuri na Yeremoti na Abia na Anatoti na Alemeti; hawa wote walikuwa wana wa Bekeri.
9Nao vichwa vya milango ya baba zao walioandikwa katika kitabu cha udugu hivyo, walivyofuatana kuzaliwa, walikuwa mafundi wa vita wenye nguvu, watu 20200.
10Nao wana wa Yediaeli: Bilihani, nao wana wa Bilihani: Yeusi na Benyamini na Ehudi na Kanaana na Zetani na Tarsisi na Ahisahari.
11Hawa wote walikuwa wana wa Yediaeli, nao walikuwa vichwa vya milango ya baba zao na mafundi wa vita wenye nguvu nyingi, watu 17200 walioweza kutoka kwenda vitani kupigana.
12Naye Supimu na Hupimu walikuwa wana wa Iri; tena Husimu na wana wa Aheri.
13Wana wa Nafutali: Yasieli na Guni na Yeseri na Salumu, ndio wana wa Biliha.[#1 Mose 46:24.]
14Wana wa Manase: Asirieli, aliyemzaa suria yake wa Kishami, ndiye aliyemzaa naye Makiri, babake Gileadi.[#4 Mose 26:29-33.]
15Naye Makiri akawaoza Hupimu na Supimu, nalo jina la umbu lake ni Maka, nalo jina la mwanawe wa pili ni Selofuhadi, naye Selofuhadi alikuwa na wana wa kike tu.[#4 Mose 27:1.]
16Naye Maka, mkewe Makiri, akazaa mwana wa kiume, akamwita jina lake Peresi, nalo jina la ndugu yake lilikuwa Seresi, nao wanawe ni Ulamu na Rekemu.
17Nao wana wa Ulamu: Bedani. Hawa ndio wana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase.
18Umbu lake Hamoleketi akazaa Ishodi na Abiezeri na Mala.
19Nao wana wa Semida: Ayani na Sekemu na Likihi na Aniamu.
20Wana wa Efuraimu: Sutela, na mwanawe huyo Beredi, na mwanawe huyo Tahati, na mwanawe huyo Elada, na mwanawe huyo Tahati,[#4 Mose 26:35.]
21na mwanawe huyo Zabadi, na mwanawe huyo Sutela, tena Ezeri na Eladi. Lakini wana wa Gati waliozaliwa katika nchi ile wakawaua, kwa kuwa walishuka kuyachukua makundi yao.
22Baba yao Efuraimu akawasikitikia siku nyingi, nao ndugu zake wakaja kumtuliza moyo.
23Kisha akaingia kwake mkewe, akapata mimba, akazaa mwana wa kiume, akamwita jina lake Beria, kwa kuwa mambo mabaya yalikuwa nyumbani mwake.
24Mwanawe wa kike ni Sera, ndiye aliyejenga Beti-Horoni wa chini na wa juu, tena Uzeni-Sera.
25Mwanawe ni Refa na Resefu, na mwanawe huyo Tela, na mwanawe huyo Tahani,
26na mwanawe huyo Ladani, na mwanawe huyo Amihudi, na mwanawe huyo Elisama,[#4 Mose 1:10.]
27na mwanawe huyo Nuni, na mwanawe huyo Yosua.[#4 Mose 13:8.]
28Nchi, waliyoichukua, iwe yao, walikokaa, ni Beteli na vijiji vyake, tena upande wa maawioni kwa jua Narani, na upande wa machweoni kwa jua Gezeri na vijiji vyake na Sekemu na vijiji vyake mpaka Gaza na vijiji vyake.[#Yos. 16:1,10.]
29Kando ya mipaka ya wana wa Manase: Beti-Seani na vijiji vyake, Taanaki na vijiji vyake, Megido na vijiji vyake, Dori na vijiji vyake. Humo ndimo, wana wa Yosefu, mwana wa Isiraeli, walimokaa.[#Yos. 17:11.]
30Wana wa Aseri: Imuna na Isiwa na Iswi na Beria, naye Sera aliyekuwa umbu lao.[#1 Mose 46:17.]
31Nao wana wa Beria: Heberi na Malkieli, huyu ndiye baba yao wa Birzaiti.
32Heberi akamzaa Yafuleti na Someri na Hotamu, naye umbu lao Sua.
33Nao wana wa Yafuleti: Pasaki na Bimuhali na Asiwati. Hawa ndio wana wa Yafuleti.
34Nao wana wa Semeri: Ahi na Roga na Huba na Aramu.
35Nao wana wa ndugu yake Helemu: Sofa na Imuna na Selesi na Amali.
36Wana wa Sofa: Sua na Harneferi na Suali na Beri na Imura,
37Beseri na Hodi na Sama na Silisa na Itirani na Bera.
38Nao wana wa Yeteri: Yefune na Pisipa na Ara.
39Nao wana wa Ula: Ara na Hanieli na Risia.
40Hawa wote walikuwa wana wa Aseri, vichwa vya milango ya baba zao, mafundi wa vita wenye nguvu nyingi waliochaguliwa, wawe vichwa vya wakuu; wao walioandikwa katika kitabu cha udugu kuwa katika vikosi vya wapiga vita hesabu yao ilikuwa watu 26000.