The chat will start when you send the first message.
1Mali zinazokutunza zitume kwenda ng'ambo ya bahari! Siku zitakapopita nyingi, utaziona tena.[#Fano. 19:17.]
2Nyingine uzigawie watu saba au wanane, kwani huyajui mabaya yatakayokuwa katika nchi.
3Mawingu yakijaa mvua huimiminia nchi. Tena mti ukiangukia upande wa kusini au wa kaskazini, basi, mahali papo hapo, mti ulipoangukia, ndipo, utakapokuwa.
4Auangaliaye upepo hatamwaga mbegu, wala ayatazamaye mawingu hatavuna.
5Kama asivyopatikana mtu anayeijua njia ya upepo, wala jinsi mifupa inavyotengenezeka kuwa mtoto tumboni mwake mwenye mimba, vivyo hivyo nawe huyajui matendo ya Mungu, anayoyatenda yote.[#Yoh. 3:6; Mbiu. 8:17.]
6Asubuhi zimwage mbegu zako, tena jioni usiulegeze mkono! Kwani hujui, kama ni hizi au ni zile zitakazofaa, au kama zote mbili pamoja zitazaa vema.
7Kweli mwanga ni mtamu, nako kuliona jua hupendeza macho.
8Kama mtu anapata miaka mingi ya kuishi, na aifurahie yote akizikumbuka siku za giza zitakazokuwa nyingi nazo; yote yatakayofuata ni ya bure.
9Wewe kijana, ufurahie utoto wako, moyo wako ule mema siku za ujana wako! Kazishike njia, moyo wako uzitakazo, kayafuate, macho yako yanayoyatazamia! Lakini ujue, ya kuwa hayo yote Mungu atakutakia shauri.[#Mbiu. 8:15.]
10Jiepushe penye masikitiko, yasiingie moyoni mwako, nayo mabaya yaangalie, yaupitie mwili wako mbali! Kwani utoto na ujana ni wa bure.