The chat will start when you send the first message.
1Kisha miaka kumi na minne ilipopita, nikapanda tena kwenda Yerusalemu pamoja na Barnaba, nikamchukua naye Tito, aende pamoja nami.[#Tume. 15:2-29.]
2Lakini nalipanda kwa kutumwa na ufunuo, nilioupata. Nikawaelezea Utume mwema, ninaowapigia wamizimu. Kupita wengine naliwaelezea wale waliowaziwa kuwa wenye cheo, wavione hivyo, ninavyovikimbilia sasa, navyo nilivyovikimbilia mbele, kama ni vya bure.[#Gal. 2:6,9.]
3Lakini hata Tito aliyekuwa pamoja nami hakushurutishwa kutahiriwa, angawa ni Mgriki.[#Tume. 16:3.]
4Lakini kulikuwako ndugu wa uwongo waliokuwa wamejiingiza na kufichaficha; hao waliingia tu, watupeleleze, tunavyomkalia Yesu Kristo pasipo mwiko wo wote, waturudishe katika utumwa wa miiko.[#Tume. 15:1,24.]
5Nasi hatukushindika, tuwatii hao, hata saa moja tu, kwamba huo Utume mwema ufulize kujulikana kuwa wa kweli.[#Gal. 3:1.]
6Lakini waliowaziwa kuwa wenye cheo hivyo, walivyo kale, si kitu kwangu, maana Mungu hatazami uso wa mtu. Nasema: Nao hao walioambiwa kuwa wenye cheo hawakuniongezea jambo;
7lakini wakaona kweli, ya kuwa mimi nimepewa kuutangaza Utume mwema kwao wasiotahiriwa, kama Petero alivyopewa kuutangaza kwao waliotahiriwa.[#Tume. 9:15; 15:12; 22:21.]
8Kwani aliyempa Petero nguvu ya kuwa mtume wao waliotahiriwa ndiye aliyenipa nami nguvu ya kuwa mtume wao wamizimu.
9Walipokitambua kipaji, nilichogawiwa, ndipo, Yakobo na Kefa na Yohana wanaowaziwa kuwa nguzo walipotupa mimi na Barnaba mikono kwamba: Tu mmoja, sisi tuipige hiyo mbiu kwao wamizimu, lakini wao kwao waliotahiriwa.[#Yoh. 1:42.]
10Walitutakia hilo moja tu, tuwakumbuke maskini wao; nami nimejipingia kulitimiza hili.[#Tume. 11:28-30; 12:25; 2 Kor. 8:9.]
11Lakini Kefa alipofika Antiokia, nikambishia usoni pake, kwani alichongewa.
12Maana kulikuwako waliotumwa na Yakobo; hao walipokuwa hawajaja bado, alikula pamoja na wamizimu. Lakini walipokuja, akatoweka na kujitenga, kwani aliwaogopa wale waliotahiriwa.[#Tume. 11:3.]
13Nao wenzake wa Kiyuda waliokuwako wakaufuata huo ujanja wake, naye Barnaba akaponzwa na huo ujanja wao.
14Lakini nilipowaona, ya kuwa hawaishiki njia nyofu wakiifuata kweli ya Utume mwema, nikamwambia Kefa mbele yao wote: Wewe u Myuda; tena mwenendo wako ni wa kimizimu, sio wa Kiyuda; imekuwaje, wewe ukiwashurutisha wamizimu kufanya mwenendo wa Kiyuda?
15Sisi tumezaliwa kuwa Wayuda, hatu wakosaji waliotoka kwao wamizimu.
16Lakini twajua: mtu hapati wongofu akiyafanya Maonyo, ila hupata wongofu akimtegemea Kristo Yesu; nasi tukamtegemea Kristo Yesu, tupate wongofu kwa kumtegemea Kristo, siko kwa kuyafanya Maonyo. Kwani hakuna aliye wa kimtu atakayepata wongofu kwa kuyafanya Maonyo.[#Tume. 15:10-11; Rom. 3:20,28; 4:5; 11:6; Ef. 2:8.]
17Lakini sisi tunaotaka kupata wongofu kwa kuwa wake Kristo, sasa wenyewe tukionekana kuwa wakosaji, je? Kristo naye siye mwenye kutumikia makosa? La, sivyo!
18Kwani nikiyajenga tena yale, niliyoyajengua, naonyesha, ya kama sipatani na mimi mwenyewe.
19Kwani hapo, niliposhindwa na Maonyo, ndipo, nilipoyafika Maonyo, nipate kumkalia Mungu, maana nimewambwa msalabani pamoja na Kristo.[#Rom. 7:6,11.]
20Tena ninaishi, lakini sasa si mimi tena ninayeishi, ila Kristo ndiye anayeishi mwilini mwangu. Maana hivyo, ninavyoishi sasa mwilini, ninaishi kwa kumtegemea Mwana wake Mungu aliyenipenda, akajitoa kwa ajili yangu.[#Gal. 1:4; Yoh. 17:23.]
21Gawio la Mungu silitangui. Kwani kama wongofu ungepatikana kwa kuyafanya Maonyo, basi, Kristo angekuwa amekufa bure.