The chat will start when you send the first message.
1Isiraeli alipokuwa kijana, nilimpenda; huko Misri ndiko, nilikomwitia mwanangu.[#2 Mose 4:22; Mat. 2:15.]
2Lakini walipowaita halafu, ndipo, walipokwenda zao na kutoka kwao hao, wakayatambikia Mabaali na kuvukizia vinyago.
3Nami mwenyewe nalimfundisha Efuraimu kwenda kwa miguu kama mtoto, nikawashika mikono, lakini hawakutambua, ya kuwa ninawaponya.
4Naliwavuta kwa kamba zimfaazo mtu na kwa vigwe vya upendo, nikawa nikiwatua mizigo mabegani pao, nikawainamia, nipate kuwalisha chakula.
5Hawatarudi katika nchi ya Misri, ila Mwasuri ndiye atakayekuwa mfalme wao, kwani wamekataa kurudi kwangu.
6Nazo panga zitazunguka mijini mwao, ziyamalize makomeo yao kwa kuyala kwa ajili ya mashauri yao.
7Walio ukoo wangu hujipingia kuniacha; wakiitwa kurudi kwake Alioko huko juu, kwao wote hakuna atakayemtukuza.
8Nitawezaje kukutoa Efuraimu au kukuacha, Isiraeli?
Nitawezaje kukutoa, uwe kama Adima (Sodomu),
au kukugeuza, uwe kama Seboimu (Gomora)?
Moyo wangu ungefudikizwa kifuani mwangu,
ungechafuka sana kwa kukuonea uchungu.
9Sitayafanya, ukali wangu wenye moto uyatakayo,
sitamwangamiza tena Efuraimu,
kwani mimi ni Mungu, si mtu;
namo katikati yenu mimi ni mtakatifu,
nisije kuingia kwenu kwa machafuko.
10Watakuja kumtafuta Bwana, atakaponguruma kama simba;
kweli atakaponguruma, ndipo, watakapokuja kwa kutetemeka
wao watoto watokao upande wa baharini.
11Watamkimbilia kama ndege kwa kutetemeka wakitoka Misri,
au kama hua wakiitoka nchi ya Asuri;
ndipo, nitakapowakalisha nyumbani mwao; ndivyo, asemavyo Bwana.