The chat will start when you send the first message.
1Njoni, tumrudie Bwana!
Yeye aliyeturarua ndiye atakayetuponya,
yeye aliyetupiga ndiye atakayetufunga vidonda.
2Ataturudisha uzimani, siku mbili zitakapopita.
Siku ya tatu atatuinua; ndipo, tutakapokuwa wazima mbele yake,
3ndipo, tutakapojua maana, tujihimize kumjua Bwana;
hana budi kutokea, kama mapambazuko yasivyokuwa na budi kutokea;
atatujia kama mvua, kama mvua ya vuli inyweshayo nchi.
4Nikufanyizie nini wewe Efuraimu?
nikufanyie nini, wewe Yuda?
Magawio yenu hufanana na wingu la asubuhi,
tena na umande unaokauka mapema.
5Kwa hiyo nimewapiga kwa wafumbuaji,
nikawaua kwa maneno ya kinywa changu,
mapatilizo yako hayana budi kutokea kama mwanga;
6kwani huruma ndizo zitazonipendeza,
vipaji vya tambiko sivyo;
kumjua Mungu hupita ng'ombe za tambiko,
ijapo ziwe za kuteketezwa nzima.
7Lakini wao kwa kimtu chao huvunja agano;
ndivyo, wanavyoniacha kwa udanganyifu.
8Gileadi ni mji wao wafanyao maovu, nyayo zao hujaa damu.
9Kama wanyang'anyi wanavyomwotea mtu,
ndivyo, chama cha watambikaji kinavyoua katika njia ya kwenda Sikemu;
ndiko, walikofanya mabaya, waliyokwisha kuyawaza.
10Kwao walio mlango wa Isiraeli nimeona mambo yazizimuayo;
ndiko, Efuraimu anakofanya ugoni, Isiraeli naye hujichafua.
11Nawe Yuda, utakayoyavuna, yako tayari;
itakuwa hapo, nitakapoyafungua mafungo yao walio ukoo wangu.