Hosea 8

Hosea 8

Makosa makubwa ya Waisiraeli.

1Weka baragumu midomoni pako kwamba:

Yuko atakayeijia Nyumba ya Bwana kama tai!

Wamelivunja Agano langu, wakayakosea Maonyo yangu.

2Watanililia kwamba: Mungu wetu, sisi Waisiraeli tunakujua!

3Lakini Isiraeli ameyatupa yaliyo mema, kwa hiyo adui atamkimbiza.

4Wameweka wafalme, nisiowaagiza mimi, wakaweka wakuu, nisiowajua!

Kwa fedha zao na kwa dhahabu zao wakajitengenezea vinyago,

kusudi viangamizwe tu.

5Ndama yako, Samaria, nimeitupa,

makali yangu yakapata kuwaka kwa ajili yao.

Mpaka lini wataweza kuendelea hivyo pasipo kutakaswa?

6Ilitokea kwao Waisiraeli, ni fundi aliyeitengeneza,

siyo Mungu, kwani itakuwa vumbi hiyo ndama ya Samaria.

7Kwa kuwa hupanda upepo, watavuna kimbunga,

mbegu zao hazioti majani, hazileti unga;

kama zingeuleta, wageni wangeula.

8Waisiraeli wamekwisha kumezwa: wako kwa wamizimu,

wanafanana na chombo kisichopendeza.

9Kwani ndio walioondoka kwenda Asuri,

wakawa kama punda wa porini anayejitembelea peke yake.

Efuraimu akajinunulia huko wagoni wampendao;

10lakini ijapo wawanunue kwa wamizimu, nitawapata na

kuwakusanya,

nao bado kidogo watagaagaa kwa kuumizwa na mizigo,

ambayo mfalme na wakuu waliwapagaza.

11Kwani Efuraimu amejipatia pengi pa kutambikia

kwa ajili ya kukosa kwao,

napo hapo pa kutambikia pakawa pao pa kukosea.

12Ijapo nimwandikie mara elfu Maonyo yangu,

huwaziwa kwake kuwa mambo mageni tu.

13Wakitoa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima hula

nyama,

Bwana hapendezwi nao; sasa atazikumbuka manza zao,

awapatilizie makosa yao, nao watarudi Misri.

14Isiraeli alipomsahau Muumbaji wake, alijenga majumba

makuu;

Yuda naye akajenga miji mingi yenye maboma.

Nami nitatia moto mijini mwake,

uyale yale majumba yake matukufu.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania