The chat will start when you send the first message.
1Nyika na nchi kavu, na mchangamke,
nalo jangwa na lipige vigelegele
kwa kuchipuka na kuchanua kama shamba la maua ya uwago.
2Litachipuka kweli na kuchanua,
lipige vigelegele na shangwe,
litapewa utukufu wa Libanoni
na urembo wa Karmeli nao wa Saroni;
hao watauona utukufu wa Bwana na urembo wa Mungu wetu.
3*Mikono iliyolegea itieni nguvu!
Nayo magoti yaliyojikwaa yashupazeni!
4Waambieni waliopotelewa na mioyo:
Jipeni mioyo, msiogope! Mtazameni Mungu wenu!
Lipizi linakuja, wanalipishwa na Mungu;
yeye ndiye atakayewaokoa ninyi.
5Hapo ndipo, yatakapofumbuliwa macho ya vipofu,
ndipo, yatakapozibuliwa masikio ya viziwi,
6ndipo, viwete watakaporukaruka kama kulungu,
ndipo, ndimi za mabubu zitakapopiga shangwe,
kwani maji yatabubujika nyikani, nayo mito jangwani.
7Mchanga wenye moto utageuka kuwa ziwa,
nayo nchi iliyokufa kwa kiu itatoka visima vya maji.
Penye makao na matuo ya mbweha
pataota nyasi na matete na magugu.
8Hata barabara iliyotengenezwa vizuri itakuwako,
nayo itaitwa Njia Takatifu;
mwenye machafu hataishika, ila itakuwa yao tu,
watakaoishika ya kukuendeako,
nao wajinga hawatapotelewa nayo.
9Simba hatakuwako kule,
wala nyama wakali wengine hawatakupanda,
hawataonekana huko kabisa.
Hivyo wale waliokombolewa wataendelea kuishika.
10Waliookolewa na Bwana watarudi,
waje Sioni na kupiga shangwe,
furaha za kale na kale zitawakalia vichwani pao,
machangamko na furaha zitawafikia,
lakini machungu yatakimbia, wasipige kite tena.*