Nehemia 10

Nehemia 10

Watu wanapata kuyashika Maonyo.

1Nao waliotia muhuri yao hi hawa: Mtawala nchi Nehemia, mwana wa Hakalia, na Sedekia;

2Seraya, Azaria, Yeremia;

3Pashuri, Amaria, Malkia;

4Hatusi, Sebania, Maluki;

5Harimu, Meremoti, Obadia;

6Danieli, Ginetoni, Baruku;

7Mesulamu, Abia, Miyamini;

8Mazia, Bilgai, Semaya; hawa ndio watambikaji.

9Nao Walawi ndio: Yesua, mwana wa Azania, Binui wa wana wa Henadadi, Kadimieli;

10na ndugu zao Sebania, Hodia, Kelita, Pelaya, Hanani;

11Mika, Rehobu, Hasabia;

12Zakuri, Serebia, Sebania;

13Hodia, Bani, Beninu.

14Wakuu wa watu ndio: Parosi, Pahati-Moabu, Elamu, Zatu, Bani;[#Ezr. 2:3,6.]

15Buni, Azgadi, Bebai;

16Adonia, Bigwai, Adini;

17Ateri, Hizikia, Azuri;

18Hodia, Hasumu, Besai;

19Harifu, Anatoti, Nobai;

20Magipiasi, Mesulamu, Heziri;

21Mesezabeli, Sadoki, Yadua;

22Pelatia, Hanani, Anaya;

23Hosea, Hanania, Hasubu;

24Halohesi, Piliha, Sobeki;

25Rehumu, Hasabuna, Masea;

26na Ahia, Hanani, Anani;

27Maluki, Harimu, Baana.

28Nao watu wengine wote, watambikaji, Walawi, walinda malango, waimbaji, watumishi wa Nyumbani mwa Mungu, nao wote waliojitenga na watu wa makabila ya nchi hizi, wayashike Maonyo ya Mungu, wake zao na wana wao wa kiume na wa kike, wote pia waliojua kuitambua maana,[#Ezr. 2:70.]

29wakawafuata ndugu zao watukufu wakijiapiza na kuapa kwamba: Tuendelee na kuyafuata Maonyo ya Mungu yaliyotolewa mkononi mwa Mose, mtumishi wake Mungu, tena tuyashike na kuyafanya maagizo yote na maamuzi yake na maongozi yake Bwana Mungu wetu.

30Tusiwape watu wa makabila ya nchi hii wana wetu wa kike, wala wana wa kike wa kwao tusiwachukue, tuwape wana wetu wa kiume,

31wala tusinunue cho chote kwao watu wa makabila ya nchi hii katika siku za mapumziko na katika siku takatifu, wakileta vyombo na vilaji kuviuza siku ya mapumziko. Tena kila mwaka wa saba tuache kulima, nayo madeni yo yote tuwaachilie watu.[#Neh. 13:15-16; Amo. 8:5.]

32Tena wakajisimamisha na kujiagiza wenyewe kutoa kila mtu kwa mwaka thumuni tatu za msaada wa kazi za Nyumba ya Mungu,

33zilipe mikate, anayowekewa Bwana, navyo vipaji vya tambiko vya kila siku nazo ng'ombe za tambiko za kila siku na za siku za mapumziko, nazo za miandamo ya mwezi, nazo za sikukuu na za siku takatifu na za Mapoza, Waisiraeli wakijitafutia upozi kwa ajili ya makosa yao, kale na kale zilipe kazi zote za Nyumba ya Mungu wetu.

34Kisha sisi watambikaji na Walawi pamoja na watu wote tukaipigia kura michango ya kuni, watakazoipelekea Nyumba ya Mungu wetu milango kwa milango ya baba zetu mwaka kwa mwaka penye siku zilizowekwa, tupate kuziteketeza ng'ombe za tambiko mezani pa Bwana Mungu wetu, kama ilivyoandikwa katika Maonyo.[#3 Mose 6:12.]

35Tena tukajisimamisha kuleta Nyumbani mwa Bwana malimbuko ya mashamba yetu na ya miti yote ya matunda mwaka kwa mwaka,[#2 Mose 23:19.]

36nao wazaliwa wa kwanza wa wana wetu na wa nyama wetu wa kufuga, kama ilivyoandikwa katika Maonyo, ndiyo malimbuko ya ng'ombe wetu na ya mbuzi na kondoo wetu, tuyapeleke Nyumbani mwa Mungu wetu kuwapa watambikaji wanaotumikia Nyumbani mwa Mungu wetu.[#2 Mose 13:2.]

37Tena tukajisimamisha kutoa malimbuko ya unga wetu wa kwanza wa kupika mikate na michango mingine itupasayo na matunda ya miti yote na mvinyo mbichi na mafuta, tuyapelekee watambikaji katika vyumba vyao vilivyopo penye Nyumba ya Mungu wetu, nao Walawi tuwapelekee mafungu ya kumi ya mashamba yetu, kwani Walawi ndio wanaoyatoza mafungu ya kumi katika miji yote, tunakolima.[#4 Mose 18:21.]

38Tena Walawi wakiyatoza mafungu ya kumi, mtambikaji aliye mwana wa Haroni sharti awe pamoja na hao Walawi, Walawi wapeleke fungu la kumi la mafungu yao ya kumi vyumbani mwa nyumba ya vilimbiko.[#4 Mose 18:26,28.]

39Kwani humo vyumbani ndimo, wana wa Isiraeli na wana wa Lawi watakamopeleka michango ya ngano na ya mvinyo mbichi na ya mafuta, kwani humo ndimo, vyombo vitakatifu vilimo, nao watambikaji na watumishi na walinda malango na waimbaji wamo mumo humo. Hatutaiacha Nyumba ya Mungu wetu, ikose cho chote.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania