The chat will start when you send the first message.
1Mtu aonwaye akishupaza shingo
mara atavunjika, asione atakayemponya.
2Waongofu wakipata nguvu, watu hufurahi,
lakini asiyemcha Mungu akitawala, watu hupiga kite.
3Mtu apendaye werevu wa kweli humfurahisha baba yake,
lakini mtu akiwa mwenzao wanawake wagoni huzipoteza mali.
4Mfalme huishikiza nchi yake kwa kupiga mashauri yaliyo sawa,
lakini aitozaye kodi nyingi huiangamiza.
5Mtu amwambiaye mwenziwe maneno mororo humtegea tanzi,
ainase miguu yake.
lakini mwongofu hupiga shangwe kwa kufurahi.
6Mtu mbaya hujitegea mwenyewe kwa upotovu wake,
lakini mwongofu hupiga shangwe kwa kufurahi.
7Mwongofu huyajua mashauri ya wanyonge,
lakini asiyemcha Mungu hautambui huo ujuzi.
8Wenye ufyozaji huuchafua mji,
lakini wenye werevu wa kweli huyatuliza makali.
9Mtu mwerevu wa kweli akishindana na mjinga,
huyu hukasirika, tena hucheka, mambo yasipate kutulia.
10Wamwagao damu humchukia asiyekosa,
lakini wanyokao hutafuta njia ya huiponya roho yake.
11Mpumbavu hutoa ukali wote wa roho yake,
lakini mwerevu wa kweli huuzuia, apate kuunyamazisha.
12Mtawalaji akisikiliza maneno ya uwongo,
watumishi wake wote huacha kumcha Mungu.
13Maskini na mkorofi hukutana,
aliyewapa wote wawili mwanga wa macho ni Bwana.
14Mfalme akataye mashauri ya wanyonge kwa kweli,
kiti chake cha kifalme kitashupaa kale na kale.
15Fimbo na mapigo humwerevusha mtu kweli,
lakini mwana aliyeachiliwa tu humtia mama yake soni.
16Wasiomcha Mungu wakipata nguvu, wapotovu huwa wengi,
lakini waongofu hufurahia maanguko yao.
17Mchape mwanao! Ndivyo, atakavyokupatia utulivu
akiifurahisha roho yako vizuri.
18Pasipo kufumbuliwa mambo watu hawazuiliki,
lakini ayaangaliaye Maonyo hufanikiwa.
19Kwa maneno tu mtumishi haonyeki,
kwani huyatambua, lakini hayatii.
20Ukiona mtu ajihimizaye kusema maneno,
basi, mpumbavu huegemeka kuliko huyo.
21Mtu akimtunza mtumishi wake kwa upole tu toka utoto,
mwisho yeye atakuwa kibwana.
22Mtu mkali huzusha magomvi,
naye akasirikaye upesi hufanya mapotovu mengi.
23Majivuno humnyenyekeza mtu,
lakini anyenyekeaye rohoni hupata macheo.
24Afanyaye bia na wezi hujichukia mwenyewe,
akisikia maapizo hamjulishi aliyeapizwa.
25Kuogopa watu ni kujitegea tanzi,
lakini amwegemeaye Bwana hulindwa.
26Wengi hutafuta upendeleo wa mtawalaji,
lakini kwake Bwana kila mtu huyapata yampasayo.
27Mtu mwovu hutapisha waongofu,
naye ashikaye njia inyokayo humtapisha asiyemcha Mungu.