The chat will start when you send the first message.
1Waisiraeli walipotoka kule Misri, wa mlango wa Yakobo walipotoka kwao wasemao msemo mgeni,[#2 Mose 12:41.]
2Ndipo, Yuda alipopata kuwa mwenye Patakatifu pao, naye Isiraeli mwenye ufalme wao.
3Bahari ilipoviona, ilikimbia, mto wa Yordani nao ukarudi nyuma.[#2 Mose 14:21-22; Yos. 3:13-16.]
4Milima ikarukaruka kama kondoo waume, navyo vilima vidogo kama wana wa kondoo.[#Sh. 68:9.]
5Wewe, bahari, ulionaje ulipokimbia? Wewe Yordani nawe, uliporudi nyuma?
6Nanyi milima, mliporukaruka kama kondoo waume? Nanyi vilima vidogo, mliporukaruka kama wana wa kondoo?
7Tetemeka, wewe nchi, Bwana akitokea, Mungu wake Yakobo akitokea mwenyewe![#2 Mose 19:18.]
8Anaugeuza mwamba kuwa ziwa la maji, nayo mawe magumu kuwa mboji za maji.[#2 Mose 17:6; 4 Mose 20:7-11.]