Mashangilio 142

Kilio cha mtu asongekaye.

1Napaza zauti, nimlilie Bwana,[#1 Sam. 24:4.]

2namlalamikia Bwana na kupaza sauti yangu.

3Mbele yake nayamwaga machozi yangu, nayo masongano yangu nayatangaza mbele yake yeye.

4Roho yangu ikitaka kuzimia kifuani mwangu, wewe unaujua mwenendo wangu, jinsi ulivyo. Njiani nipitapo wamenitegea matanzi;

5ukitazama kuumeni utaona, hakuna anikaguaye. Nimepotelewa na kimbilio, hakuna aniulizaye.[#Sh. 138:7.]

6Nimekupalizia sauti, Bwana, nikasema kwamba: Wewe u kimbilio langu na fungu langu nchini kwao walio hai.

7Yaangalie malalamiko yangu! Kwani nimekorofika sana. Niopoe kwao wanikimbizao! Kwani nguvu zao hunishinda.[#Sh. 27:13.]

8Itoe roho yangu kifungoni, ilishukuru Jina lako! Waongofu watanizunguka, ukinitendea mema.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania