The chat will start when you send the first message.
1Bwana, tazama, jinsi walivyo wengi wanaonisonga! Tena ni wengi wanaoniinukia.[#2 Sam. 15:14.]
2Ndio wengi wanaoiwazia roho yangu ya kwamba: Hapana wokovu, atakaoupata kwake Mungu.
3Lakini wewe Bwana, u ngao inikingiayo, kwa kuwa utukufu wangu utakikweza kichwa changu.[#Sh. 84:12.]
4Ninapoipaza sauti yangu, ifike kwake Bwana, huniitikia toka mlimani kwenye utakatifu wake.
5Mimi nililala usingizi, kisha nikaamka, kwani mwenye kunishikiza ni Bwana.[#Sh. 4:8; Fano. 3:24.]
6Ijapo, watu wawe maelfu na maelfu, siwaogopi, wakija kunipangia na kunizunguka.[#Sh. 27:3.]
7Inuka, Bwana! Niokoe, Mungu wangu! Kwani walio adui zangu unawapiga makofi wote, ukawavunja meno wasiokucha, wewe.[#Sh. 58:7.]
8Kwako Bwana uko wokovu, uwapatie mema wao walio ukoo wako.[#Yer. 3:23.]