Mashangilio 5

Mashangilio 5

Maombo ya asubuhi kwa kulindiwa wabaya.

1Bwana, yasikilize maneno yangu! Yatambue nayo manong'ono yangu!

2Sauti ya kilio changu itegee masikio! Mfalme wangu na Mungu wangu, ninakulalamikia.[#Sh. 84:4.]

3Bwana, asubuhi uisikie sauti yangu! Asubuhi ninajiweka kuwa tayari, nikuchungulie.

4Kwani wewe siwe Mungu apendezwaye naye asiyekucha, wala mtu mbaya hakai huko, uliko.

5Wajitukuzao hawasimami machoni pako; unawachukia wote wafanyao maovu.

6Utawaangamiza kabisa wao wasemao uwongo, wenye kiu ya damu na wadanganyaji humtapisha Bwana.

7Lakini mimi kwa wingi wa upole wako nitaingia Nyumbani mwako, nikuangukie Patakatifu pako pa kuombea, kwa maana ninakuogopa.[#Sh. 26:8.]

8Bwana, niongoze, niufuate wongofu wako, kwa ajili yao waninyatiao, ukainyoshe njia yako machoni pangu!

9Kwani vinywani mwao hao hamna yaliyo sawa, mioyoni mwao hukaa tamaa mbaya tu, makoo yao huwa makaburi yaliyo wazi, ndimi zao nazo huteleza.[#Rom. 3:13.]

10Wapatilize, Mungu, waangushwe na mashauri yao, wakumbe kwa ajili ya maovu yao mengi! Kwani wamekubisha.

11Wote wakuegemeao wapate kufurahi kale na kale, wapige vigelegele, kwani huwakingia, wakushangilie wote walipendao Jina lako![#Sh. 40:17.]

12Kwani wewe, Bwana, unambariki aliye mwongofu, ukamvika upendelevu, kama ni ngao.[#Sh. 103:4.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania