The chat will start when you send the first message.
1Kisha nikaona malaika mwingine mwenye nguvu aliyeshuka toka mbinguni; vazi lake lilikuwa wingu, kofia la kichwani pake lilikuwa upindi wa Mungu, uso wake ulikuwa kama jua, miguu yake ilikuwa kama nguzo zenye moto.[#Ufu. 5:2; 4:3.]
2Mkononi mwake alishika kitabu kidogo kilichokuwa kimefunuka. Mguu wake wa kuume ulikanyaga juu ya bahari, wa kushoto juu ya nchi.[#Ufu. 5:1.]
3Akapaza sauti kuu, kama simba anavyolia. Naye alipopaza sauti, ngurumo saba zilizitoa sauti zao.[#Yer. 25:30; Hos. 11:10; Amo. 1:2.]
4Hizo ngurumo saba zilipokwisha sema, nalitaka kuandika. Ndipo, niliposikia sauti toka mbinguni, ikisema: Yafiche na kuyatia muhuri, hizo ngurumo saba ziliyoyasema, lakini usiyaandike![#Dan. 8:26; 12:4,9.]
5Naye malaika, niliyemwona, alivyosimama mguu mmoja baharini na mmoja nchini, akauelekeza mkono wake wa kuume mbinguni,
6akaapa na kumtaja yeye aliye Mwenye uzima kale na kale pasipo mwisho, aliyeziumba mbingu navyo vilivyomo ndani yake, hata nchi navyo vilivyomo ndani yake, hata bahari navyo vilivyomo ndani yake, akisema: Hapatakuwa siku tena,[#Ufu. 6:11; Dan. 12:7.]
7ila siku ya sauti ya malaika wa saba, atakapopiga baragumu, ndipo, patakapotimia fumbo la Mungu, kama alivyowapigia mbiu njema wale wafumbuaji waliokuwa watumwa wake.[#Ufu. 11:15; 17:17; Tume. 3:21.]
8Ndipo, ile sauti, niliyoisikia toka mbinguni, iliposema tena nami kwamba: Nenda, ukitwae kile kitabu kidogo kilichokuwa kimefunuka, kilichomo mkononi mwa malaika aliyesimama mguu mmoja baharini na mmoja nchini![#Ufu. 10:2,4.]
9Nikaenda kwa yule malaika, nikamwambia, anipe kile kitabu kidogo. Naye akaniambia: Kitwae, kile! Kitakutia uchungu tumboni mwako, lakini kinywani mwako kitakuwa kitamu kama asali.[#Ez. 3:1-4.]
10Nikakitwaa kile kitabu kidogo mkononi mwa yule malaika, nikakimeza, nacho kilikuwa kitamu kama asali kinywani mwangu; lakini nilipokwisha kukimeza nikatiwa uchungu tumboni mwangu.
11Wakaniambia: Wewe imekupasa kufumbulia tena makabila mengi na wamizimu wengi na wenye misemo mingi na wafalme wengi.