The chat will start when you send the first message.
1Malaika wa wateule walioko Sarde mwandikie: Ndivyo anavyosema yeye aliye mwenye zile roho saba za Mungu na mwenye zile nyota saba. Nayajua matendo yako, unalo jina la kuwa unaishi, lakini u mfu.[#Ufu. 1:16; 5:6.]
2Amka, uyashupaze masao yanayotaka kufa nayo! Kwani sikuyaona matendo yako, ya kuwa yametimilika mbele ya Mungu wangu.[#Ufu. 3:19; Ez. 34:4.]
3Kumbuka, uliyoyapokea! Nayo uliyoyasikia, yashike, upate kujuta! Usipokesha, nitakuja kama mwizi, usiitambue saa, nitakayokujia wewe.[#1 Tes. 5:2.]
4Lakini unayo majina machache huko Sarde wasiozichafua nguo zao. Ndio watakaoenenda pamoja nami wenye nguo nyeupe, kwani zimewapasa.[#Yuda 23.]
5Mwenye kushinda atavikwa naye nguo nyeupe, nalo jina lake sitalifuta katika kitabu cha uzima. Nami nitaliungama jina lake mbele ya Baba yangu na mbele ya malaika zake.[#Ufu. 4:4; 6:11; 7:9,13; Sh. 69:29; Mat. 10:32; Fil. 4:3.]
6Mwenye masikio na asikie, Roho anayowaambia wateule!
7Malaika wa wateule walioko Filadelfia mwandikie: Ndivyo, anavyosema yeye Mtakatifu aliye mwenye kweli, aliye hata mwenye ufunguo wa Dawidi. Atakapofungua, hatakuwako awezaye kupafunga tena; atakapofunga, hatakuwako awezaye kupafungua.[#Yes. 22:22.]
8Nayajua matendo yako, tazama mbele yako nimekupa mlango ulio wazi, tena hakuna awezaye kuufunga. Kweli nguvu, ulizo nazo, ni ndogo, lakini umelishika Neno langu, hukulikana Jina langu.[#1 Kor. 16:9.]
9Tazama, nitakupa wanafunzi wa Satani wanaojisema kuwa Wayuda, lakini sio, ila husema uwongo. Tazama, nitawaleta hao, waje, wakuangukie penye miguu yako, watambue, ya kuwa mimi nimekupenda wewe.[#Ufu. 2:9; Yes. 49:23; 60:14.]
10Kwa sababu umelishika Neno langu la uvumilivu, nitakulinda nami, nikuokoe katika saa ya majaribu itakayopafikia pote panapokaa watu kwamba: Wakaao nchini wajaribiwe.[#Ufu. 13:10; Rom. 8:25; 1 Kor. 10:13; Ebr. 10:36.]
11Ninakuja upesi. Shikamana nayo, uliyo nayo, mtu asikitwae kilemba chako![#Ufu. 1:3; 2:5,10.]
12Mwenye kushinda nitamfanya kuwa nguzo Jumbani mwa Mungu wangu, asitoke tena nje. Nami nitamwandika Jina la Mungu wangu na jina la mji wa Mungu wangu, la Yerusalemu mpya, utakaoshuka toka mbinguni kwake Mungu wangu. Nitamwandika hata Jina langu jipya.[#Ufu. 14:1; 19:12; 21:2; 22:4; Yes. 62:2; Gal. 2:9; 4:26.]
13Mwenye masikio na asikie, Roho anayowaambia wateule!
14Malaika wa wateule walioko Laodikia mwandikie: Ndivyo, anavyosema yeye Amin aliye shahidi mwelekevu na mkweli, aliye wa kwanza wa viumbe vyote vya Mungu.[#Ufu. 1:5; Yoh. 1:3; 2 Kor. 1:20; Kol. 1:15.]
15Nayajua matendo yako, wewe huzizimiki, wala huzizimuki. Ungefaa ukiwa mwenye kuzizimika au mwenye kuzizimuka.[#Ufu. 2:2.]
16Lakini sasa, kwa kuwa u mwenye kuvuvuwaa, usiwe mwenye kuzizimika wala mwenye kuzizimuka, nitakutema kinywani mwangu.
17Kwani unasema: Mimi niko na mali, ninayo malimbiko yangu, hakuna, nilichokikosa. Nawe hujui, ya kuwa wewe u mnyonge, unapaswa na kugawiwa, u maskini na kipofu na mwenye uchi.[#1 Kor. 3:18; 4:8.]
18Nakuonyesha mzungu, ndio huu: nunua kwangu dhahabu iliyong'azwa na moto, upate kuwa mwenye mali! Nunua nazo nguo nyeupe, upate kuvaa, uchi wako usionekane, ukakutia soni! Nunua nayo mafuta ya macho, uyapake macho yako, upate kuona![#Ufu. 16:15; Yes. 55:1; 1 Petr. 1:7.]
19Wote, ninaowapenda mimi, nawaonya na kuwapiga. Kwa hiyo jikaze, ujute![#Fano. 3:12; 1 Kor. 11:32; Ebr. 12:6.]
20Tazama, nimesimama mlangoni nikipiga hodi. Mtu atakayenisikia sauti yangu, akaufungua mlango, basi, nitaingia mwake, nile pamoja naye, naye ale pamoja nami.[#Luk. 12:36; Yoh. 14:23.]
21Mwenye kushinda nitampa kukaa pamoja nami kitini pangu pa kifalme, kama mimi nami nilivyoshinda, nikakaa pamoja na Baba yangu kitini pake pa kifalme.[#Mat. 19:28.]
22Mwenye masikio na asikie, Roho anayowaambia wateule!