The chat will start when you send the first message.
1Tazama, jicho langu limeyaona hayo yote,
Sikio langu limeyasikia na kuyaelewa.
2Hayo myajuayo ninyi, na mimi pia nayajua;
Mimi si duni kuliko ninyi.
3Hakika ningenena naye huyo Mwenyezi,
Nami nataka kuhojiana na Mungu.
4Lakini ninyi hubuni maneno ya uongo,
Ninyi nyote ni matabibu wasiofaa.
5Laiti mngenyamaza kabisa![#Mit 17:28; Mhu 5:3; Amo 5:13; Yak 1:19]
Hilo lingekuwa hekima kwenu.
6Sikieni sasa basi hoja zangu,
Mkayasikie malalamiko ya midomo yangu.
7Je! Mtanena yasiyo ya haki kwa ajili ya Mungu,[#Ayu 17:5; Rum 3:5,8]
Na kusema kwa udanganyifu kwa ajili yake?
8Je! Mtamwonesha yeye upendeleo?[#Mit 24:23]
Mtamtetea Mungu?
9Je! Itafaa yeye kuwatafuta ninyi?
Au, kama kumdanganya mtu, je! Mtamdanganya yeye?
10Hakika atawakemea ninyi,
Mkiwapendelea watu kwa siri.
11Je! Huo ukuu wake hautawatia hofu,
Na utisho wake hautawaangukia?
12Maneno yenu ya hekima ni mithali ya majivu,
Ngome zenu ni ngome za udongo.
13Nyamazeni, niacheni, ili nipate kunena,
Na hayo yatakayonijia na yaje.
14Nitaitwaa nyama ya mwili wangu katika meno yangu,[#Zab 119:109]
Na kuutwaa uhai wangu mkononi mwangu!
15Tazama, ataniua; sina tumaini;[#Zab 23:4; Mit 14:32; Rum 8:38,39; Ayu 27:5; #13:15 Au, ajaponiua, nitamngojea vivyo.]
Ila hata hivyo nitaithibitisha njia yangu mbele yake.
16Hili nalo litakuwa ni wokovu wangu;[#Isa 12:1,2]
Kwani asiyemcha Mungu hatakaribia mbele yake.
17Sikieni sana maneno yangu,
Maelezo yangu na yaingie masikioni mwenu.
18Angalieni sasa, nimekwisha kulitengeneza neno langu,
Najua ya kuwa mimi ni mwenye haki.
19Yuko nani atakayeshindana nami?[#Ayu 33:6; Isa 50:8]
Maana sasa nitanyamaza kimya na kukata roho.
20Lakini msinifanyie mambo mawili, hayo tu,
Ndipo nami sitajificha usoni pako;
21Uondoe mkono wako usinilemee;
Na utisho wako usinitie hofu.
22Basi uite wakati huo, nami nitaitika;
Au, niache ninene mimi, nawe unijibu.
23Maovu yangu na dhambi zangu ni ngapi?
Nijulishe kosa langu na dhambi yangu.
24Mbona umeuficha uso wako,[#Zab 10:1; Isa 8:17; Omb 2:5; 2 The 3:15]
Na kunihesabu kuwa ni adui yako?
25Je! Utalitaabisha jani lipeperushwalo?[#Isa 17:13; 42:3]
Au, je! Utayafuatia hayo mabua makavu?
26Kwani umeandika maneno ya uchungu juu yangu,[#Zab 25:7]
Na kunirithisha maovu ya ujana wangu;
27Waitia miguu yangu katika mkatale, na kuyakagua mapito yangu yote;[#Ayu 33:11]
Wajiandikia alama kuzizunguka nyayo za miguu yangu;
28Nijapokuwa ni kama kitu kilichooza, kinachosinyaa,
Mfano wa nguo iliyoliwa na nondo.