The chat will start when you send the first message.
1Kisha wana wa Israeli wakasafiri na kupanga katika nchi tambarare za Moabu ng'ambo ya pili ya Yordani karibu na Yeriko.[#Hes 33:48; Mwa 35:5; Kut 23:27; Kum 2:25; Yos 2:9; Yer 32:21]
2Na Balaki mwana wa Sipori akaona mambo yote ambayo Israeli wamewatendea Waamori.[#Amu 11:25]
3Moabu akawaogopa hao watu sana, kwa kuwa walikuwa wengi; Moabu akafadhaika kwa sababu ya wana wa Israeli.[#Kut 15:15]
4Moabu akawaambia wazee wa Midiani, Sasa jeshi hili la watu litaramba vitu vyote vinavyotuzunguka, kama vile ng'ombe arambavyo majani ya mashamba. Na Balaki, mwana wa Sipori, alikuwa mfalme wa Moabu zamani zile.[#Hes 31:8; Yos 13:21]
5Basi akatuma wajumbe kwa Balaamu mwana wa Beori, hadi Pethori, ulio kando ya Mto, mpaka nchi ya wana wa watu wake, kwenda kumwita, akisema, Tazama, kuna watu waliotoka Misri; tazama, wanaufunika uso wa nchi, tena wanakaa kunikabili mimi.[#Hes 31:8; 2 Pet 2:15-16; Yud 11; Kum 23:4; Yos 13:22; Neh 13:1,2; Mik 6:5]
6Basi, njoo wewe, nakusihi unilaanie watu hawa; maana wana nguvu kunishinda mimi. Labda nitawaweza, tupate kuwapiga, niwafukuze watoke katika nchi yangu, kwa maana najua ya kuwa yeye umbarikiye hubarikiwa, na yeye umlaaniye hulaaniwa.[#Mwa 12:3; 27:29; Hes 23:7; Kum 23:4; Yos 24:9; 1 Sam 17:43; Neh 13:2]
7Wazee wa Moabu, na wazee wa Midiani, wakaenda, wakichukua ujira wa uganga mikononi mwao; wakamfikia Balaamu, wakamwambia maneno ya Balaki.[#Kut 23:8; 1 Sam 9:7,8; Mit 17:23; Isa 56:11; Mik 3:11]
8Akawaambia, Kaeni hapa usiku huu, nami nitawaletea jawabu kama BWANA atakavyoniambia; wakuu wa Moabu wakakaa na Balaamu.
9Mungu akamjia Balaamu, akasema, Ni watu gani hawa ulio nao pamoja nawe?[#Mwa 20:3; 31:24]
10Balaamu akamwambia Mungu, Balaki mwana wa Sipori, mfalme wa Moabu, amewatuma kwangu, akisema,
11Tazama, kuna watu waliotoka Misri, wanaufunika uso wa nchi; basi njoo unilaanie watu hawa; labda nitaweza kupigana nao, na kuwafukuza.
12Mungu akamwambia Balaamu, Usiende pamoja nao; wala usiwalaani watu hawa, maana wamebarikiwa.[#Mwa 12:2; 22:17; 28:13,14; Hes 23:20; Kum 23:5; 33:29; Zab 144:15; Rum 11:29]
13Balaamu akaondoka asubuhi akawaambia wakuu wa Balaki, Nendeni zenu hadi nchi yenu; kwa maana BWANA amekataa kunipa ruhusa niende pamoja nanyi.
14Wakuu wakaondoka wakaenda kwa Balaki, wakasema, Balaamu, anakataa kuja pamoja nasi.
15Basi Balaki akatuma wakuu mara ya pili, wengi zaidi, wenye cheo cha juu kuliko wale wa kwanza.
16Wakamfikia Balaamu, wakamwambia, Balaki mwana wa Sipori asema hivi, Nakusihi, neno lolote lisikuzuie usinijie;
17maana nitakutunukia heshima kubwa sana, na neno lolote utakaloniomba nitalitenda; basi njoo, nakusihi, unilaanie watu hawa.[#Kum 16:19; Zab 49:17; Mt 4:8,9; 16:26]
18Balaamu akajibu akawaambia watumishi wa Balaki, Hata kama Balaki angenipa nyumba yake imejaa fedha na dhahabu, siwezi kukiuka neno la BWANA, Mungu wangu, kulipunguza au kuliongeza.[#1 Fal 22:14; 2 Nya 18:13]
19Basi sasa nawasihi, kaeni hapa tena usiku huu, nipate kujua BWANA atakaloniambia zaidi.
20Mungu akamjia Balaamu usiku, akamwambia, Kwa kuwa watu hawa wamekuja kukuita, nenda pamoja nao; lakini neno lile nitakalokuambia ndilo utakalolitenda, basi.[#Hes 23:12,26; 24:13; Zab 33:10,11; Isa 37:29; 46:10]
21Balaamu akaondoka asubuhi, akatandika punda wake, akaenda pamoja na wakuu wa Moabu.[#Mit 15:27; 1 Tim 6:9,10; 2 Pet 2:15; Yud 1:11]
22Hasira ya Mungu ikawaka kwa sababu alikwenda; malaika wa BWANA akajiweka njiani, ili kumpinga. Basi alikuwa amepanda punda wake, na watumishi wake wawili walikuwa pamoja naye.[#Kut 4:24; 23:20]
23Na yule punda akamwona malaika wa BWANA amesimama njiani, na upanga wake mkononi mwake amekwisha kuufuta; punda akageuka upande ili kuiacha njia, akaingia shambani. Balaamu akampiga punda ili kumrejesha njiani.[#2 Fal 6:17]
24Kisha malaika wa BWANA akasimama mahali penye bonde, katikati ya mashamba ya mizabibu, tena penye kitalu upande huu na kitalu upande huu.
25Yule punda akamwona malaika wa BWANA, akajisukuma ukutani, akaubana mguu wake Balaamu, basi akampiga mara ya pili.[#Isa 47:12; 1 Kor 3:19]
26Malaika wa BWANA akaenda mbele akasimama mahali pembamba sana, hapakuwa na nafasi ya kugeukia mkono wa kulia, wala mkono wa kushoto.[#Isa 26:11; Hos 2:6]
27Yule punda akamwona malaika wa BWANA, akajilaza chini ya Balaamu; hasira yake Balaamu ikawaka, akampiga punda kwa fimbo yake.[#Mit 14:16; 27:3,4; Yak 1:19]
28BWANA akakifunua kinywa cha yule punda, naye akamwambia Balaamu, Nimekutenda nini, hata ukanipiga mara tatu hizi?[#Mt 19:26; 1 Kor 1:19; 2 Pet 2:16]
29Balaamu akamwambia punda; Kwa sababu umenidhihaki; laiti ningekuwa na upanga mkononi mwangu ningekuua sasa hivi.[#Mit 12:10; Mhu 9:3; Yer 17:9; Mt 15:19]
30Yule punda akamwambia Balaamu, Je! Mimi si punda wako, nawe umenipanda maisha yako yote hata leo? Nimezoea kukutenda hayo? Akasema, La![#1 Kor 1:27]
31Ndipo BWANA akafunua macho ya Balaamu akamwona malaika wa BWANA amesimama njiani, akiwa na upanga mkononi mwake, umekwisha kufutwa, naye akainamisha kichwa, akaanguka kifudifudi.[#Mwa 21:19; 2 Fal 6:17; 1 Nya 21:16; Lk 24:16; Ayu 8:20; Mit 11:2; Yer 3:25]
32Malaika wa BWANA akamwambia, Mbona umempiga punda wako mara tatu hizi? Tazama mimi nimekuja ili kukupinga, kwa sababu njia yako imepotoka mbele zangu,[#Kum 23:4; Mit 28:6; Mik 6:5; Mdo 13:10; 2 Pet 2:14,15; #22:32 ‘Au njia yako ni mbaya’.]
33punda akaniona, akageuka upande mbele zangu mara tatu hizi; kama asingejiepusha nami, bila shaka ningalikuua wewe, nikamwacha yeye hai.
34Balaamu akamwambia malaika wa BWANA, Nimefanya dhambi; maana sikujua ya kuwa wewe umesimama njiani ili kunipinga; basi sasa, ikiwa umechukizwa, nitarudi tena.[#1 Sam 26:21; 2 Sam 12:13]
35Malaika wa BWANA akamwambia Balaamu Nenda pamoja na watu hawa, lakini neno lile nitakalokuambia, ndilo utakalosema. Basi Balaamu akaenda pamoja na wakuu wa Balaki.
36Balaki aliposikia ya kuwa Balaamu amefika, akatoka kwenda kumlaki, mpaka Mji wa Moabu, ulioko katika mpaka wa Arnoni, ulioko katika upande wa mwisho wa mpaka huo.[#Mwa 14:17; 18:2; Kut 18:7; 1 Sam 13:10; Mdo 28:15]
37Balaki akamwambia Balaamu, Je! Mimi sikutuma watu kwako kwa bidii ili kukuita? Mbona hukunijia? Je! Siwezi mimi kukufanyizia heshima nyingi?
38Balaamu akamwambia Balaki, Tazama, nimekujia. Je! Mimi sasa nina uwezo wowote kusema neno lolote? Neno lile Mungu atakalolitia kinywani mwangu, ndilo nitakalolisema.[#1 Fal 22:14; 2 Nya 18:13]
39Balaamu akaenda pamoja na Balaki wakafika Kiriath-husothi.
40Balaki akachinja ng'ombe, na kondoo, akampelekea Balaamu na wale wakuu waliokuwa pamoja naye.
41Ikawa asubuhi Balaki akamchukua Balaamu, akampandisha hadi Bamoth-baali; na kutoka huko aliweza kuwaona baadhi ya Waisraeli hadi pande zao za mwisho.[#Kum 12:2; 2 Nya 11:15; Yer 48:35; #22:41 Katika Kiebrania ni akawaona watu.]