The chat will start when you send the first message.
1Heri amkumbukaye mnyonge;[#Mit 14:21; Mk 10:21; #41:1 Au maskini.]
BWANA atamwokoa siku ya taabu.
2BWANA atamlinda na kumhifadhi hai,
Naye atafanikiwa katika nchi;
Wala usimtie katika hali wamtakiayo adui zake.
3BWANA atamtegemeza alipo mgonjwa kitandani.
Katika ugonjwa wake unamponya maradhi yake yote.
4Nami nilisema, BWANA, unifadhili,[#Zab 6:2]
Uniponye roho yangu maana nimekutenda dhambi.
5Adui zangu wananitaja kwa maneno mabaya,
Atakufa lini, jina lake lipotee?
6Na mmoja wao akija kunitazama asema uongo,[#Zab 12:2]
Moyo wake hujikusanyia maovu,
Naye atokapo nje huyanena.
7Wote wanaonichukia wananong'onezana juu yangu,
Wananiwazia yaliyo mabaya zaidi.
8Wanafikiri pigo liualo limemshika,
Akalala asiweze kusimama tena.
9Hata rafiki yangu mwandani niliyemtumaini,[#Mt 26:23; Oba 1:7; Mk 14:18; Lk 22:21; Yn 13:18]
Aliyekula pamoja nami,
Ameniinulia kisigino chake.
10Lakini Wewe, BWANA, unifadhili,
Uniinue nipate kuwalipa.
11Kwa neno hili nimejua ya kuwa wapendezwa nami,
Kwa kuwa adui yangu hajivunii kunishinda.
12Nami katika ukamilifu wangu umenitegemeza,[#Zab 34:15; Mdo 2:28]
Umeniweka mbele za uso wako milele.
13Na atukuzwe BWANA, Mungu wa Israeli,[#Zab 106:48]
Tangu milele hata milele. Amina na Amina.