The chat will start when you send the first message.
1Mungu asimama katika kusanyiko la Mungu;[#Mhu 5:8; Kut 21:6]
Katikati ya miungu anahukumu.
2Hadi lini mtahukumu kwa dhuluma,[#Kum 1:17; Zab 58:1,2]
Na kuzikubali nyuso za wabaya?
3Mfanyieni hukumu maskini na yatima;
Mtendeeni haki aliyeonewa, na fukara;
4Mwokoeni maskini na mhitaji;
Mwopoeni mikononi mwa wadhalimu.
5Hawajui wala hawafahamu, hutembea gizani;[#Zab 11:3]
Misingi yote ya nchi imetikisika.
6Mimi nimesema, Ndinyi miungu,[#Ayu 21:32; Eze 31:14; Yn 10:34]
Na wana wa Aliye Juu, enyi nyote.
7Lakini mtakufa kama wanadamu,
Mtaanguka kama mmoja wa wakuu.
8Ee Mungu, usimame, uihukumu nchi,[#Zab 2:8; Ufu 11:15]
Maana mataifa yote ni yako.