The chat will start when you send the first message.
1MTU na atubesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu.
2Tena inayohitajiwa katika mawakili, ndio mtu aonekane amini.
3Kwangu, lakini, si kitu kabisa nibukumiwe na ninyi, ama na hukumu ya kibinadamu, wala sijihukumu hatta nafsi yangu.
4Maana sijui sababu ya kujishitaki nafsi yangu, lakini sihesabikiwi haki kwa ajili hiyo; illa aninukumuye ni Bwana.
5Bassi msihukumu neno kabla ya wakati wake, mpaka ajapo Bwana; nae atayamulika yaliyosetirika ya giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo killa mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.
6Mambo haya, ndugu, nimeyafanya kuwa mfano wa mimi na wa Apollo kwa ajili yemi, illi kwa khabari zetu mpate kujifunza katika fikara zenu kutokuruka mpaka wa yale yaliyoandikwa; mtu mmoja asijivune juu ya mwenziwe, kwa ajili ya mtu mwingine.
7Maana ni nani anaekupambanua na mwingine? na una, nini usiyoipokea? Na iwapo uliipokea, wajisifiani kana kwamba hukuipokea?
8Mmekwisha kushiba, mmekwisha kupata utajiri, mmemiliki pasipo sisi. Na ingekuwa kheri kama mngalimiliki, illi sisi nasi tumiliki pamoja nanyi.
9Maana nadhani ya ku wa Mungu ametutoa sisi mitume mwisho kama watu waliohukumiwa wauawe; kwa sababu tumekuwa tamasha kwa dunia na malaika na wana Adamu.
10Sisi tu wapumbavu kwa ajili ya Kristo, lakini ninyi wenye akili katika Kristo; sisi dhaifu, lakini ninyi hodari; ninyi mna utukufu, lakini sisi hatupati heshima.
11Hatta saa hii ya sasa, tuna njaa na kiu, tu uchi, twapigwa makofi, hatuna makao;
12tena twataabika tukifanya kazi kwa mikono yetu wenyewe. Tukitukanwa twabariki, tukiudhiwa twavumilia;
13tukisingiziwa twasihi: tumefanywa kama takataka za dunia, na kifusi cha vitu vyote hatta sasa.
14Siyaandiki haya illi kuwatahayarisha, hali kuwaonya kama watoto niwapendao. Maana ijapokuwa mna waalimu elfu katika Kristo, illakini hamna baba wengi.
15Maana mimi ndiye aliyewazaa katika Kristo Yesu kwa Injili.
16Bassi, nawasihini, mwe wafuasi wangu.
17Kwa hiyo nalimtuma Timotheo kwenu, aliye mwana wangu mpendwa, mwaminifu katika Bwana, atakaewakumbusha njia zangu zilizo katika Kristo, kama nifundishavyo killa pahali katika killa kanisa.
18Wengine wamejivuna kana kwamba siji kwenu.
19Lakini nitakuja kwemi upesi, Bwana akipenda, nami nitajua, si neno lao waliojivuna, bali nguvu zao.
20Maana ufalme wa Mungu hauwi katika neno, hali katika nguvu.
21Mnataka nini? Nije kwenu na fimbo, au katika upendo na roho ya upole?