The chat will start when you send the first message.
1USIMKEMEE mzee, bali mwonye kama baba, na wadogo wako kama ndugu:
2wanawake wazee kama mama, wanawake vijana kama ndugu, kwa utakatifu wote.
3Waheshimu wajane walio wajane kweli kweli.
4Lakini mjane akiwa ana watoto au wajukuu, na wajifunze kwanza kutenda yaliyo wajib wao katika nyumba yao wenyewe, na kuwalipa wazazi wao. Maana jambo hili ni zuri, tena lipendezalo mbele za Mungu.
5Bali yeye aliye mjane kweli kweli, na kuachwa peke yake, amemwekea Mungu tumaini lake, nae hudumu katika maombi na sala mchana na usiku.
6Na yeye asiyejizuia nafsi yake amekufa ingawa yu hayi.
7Uwaagize haya, illi wawe bawana lawama.
8Lakini mtu asiyewatunza walio wake na khassa watu wa nyumba yake ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko yeye asiyeamini.
9Mjane aandikwe, ikiwa umri wake amepata miaka sittini, isipungue, nae amekuwa mke wa mume mmoja,
10na kushuhudiwa kwa matendo mema; ikiwa amelea watoto, ikiwa amekaribisha wageni, ikiwa amewaosha watakatifu miguu, ikiwa amewasaidia wateswao, ikiwa amefuata killa tendo jema.
11Bali wajane walio vijana nkatae kuwaandika, maana wakiona tamaa kinyume cha Kristo, wataka kuolewa,
12nao wana hukumu, kwa kuwa wameiacha imani yao ya kwanza.
13Na pamoja na hayo wajifunza kuwa wavivu, wakizungukazunguka nyumba kwa nyumba; wala si wavivu tu, lakini ni wachongezi, hujishughulisha na mambo ya wengine wakinena maneno yasiyowapasa.
14Bassi napenda wajane wasio wazee waolewe, wazae watoto, watawale mambo ya nyumbani, wasimpe adui nafasi ya kulaumu;
15maana wengine wamekwisha kugeuka na kumfuata Shetani.
16Mwanamume au mwanamke aamimye, akiwa na wajane, awasaidie, kanisa lisilemewe; illi liwasaidie wale walio wajane kweli kweli.
17Wazee watawalao vema wapewe heshima mardufu, khassa wao wajitaabishao kwa kukhutubu na kufundisha.
18Kwa maana andiko lasema, Usimfunge kinywa ngʼombe apurapo nganu: na tena, Mtenda kazi astahili ujira wake.
19Usikubali mashitaka juu ya mzee, illa kwa vinywa vyao mashahidi wawili au watatu.
20Wale watendao dhambi, uwakemee mbele ya watu wote, illi na wengine waogope.
21Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Bwana Kristo Yesu, na mbele ya malaika wateule, yatende hayo pasipo kuhukumu kwa haraka; usifanye neno lo lote kwa upendeleo.
22Usimwekee mtu mikono kwa haraka, wala usishiriki dhambi za watu wengine.
23Jilinde nafsi yako uwe safi; tokea sasa usinywe maji tu, bali tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo marra nyingi.
24Dhambi za watu wengine ni dhahiri, zatangulia kwenda hukumuni; wengine dhamhi zao zawafuata.
25Vivyo hivyo matendo mazuri ni dhahiri; na yale yasiyo dhahiri hayawezi kusetiriwa.