The chat will start when you send the first message.
1BASSI tunakusihini, ndugu, katika khabari ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na kukusanyika kwetu mbele yake,
2msifadhaishwe upesi na kuaeha nia yenu, wala msistushwe, kwa roho wala kwa neno, wala kwa waraka unaodhaniwa kuwa ni wetu, ya kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwapo.
3Mtu aliye yote asiwadanganye kwa njia yo yote, maana haiji isipokuja kwanza ile faraka, akafumiliwa yule mtu wa dhambi, mwana wa uharibifu,
4yule mpingamizi, ajiinuae nafsi yake juu ya killa kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hatta yeye mwenyewe huketi katika hekalu la Mungu, kama Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba ndive Mungu.
5Hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwa pamoja nanyi naliwaambieni hayo?
6Na sasa lizuialo mwalijua, apate kufunuliwa huyu wakati wake. Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi;
7lakini yuko azuiae sasa, hatta atakapoondolewa.
8Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambae Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa mafunuo ya kuwako kwake;
9ambae kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kazi kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za nwongo,
10na katika madanganya yote ya udhalimu kwao wanaopotea: kwa sababu hawakukubali kuipenda kweli, wapate kuokolewa.
11Kwa biyo Mungu atawaletea nguvu ya upotevu, wauamini uwongo,
12illi wahukumiwe wote wasioamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu.
13Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, ndugu, mliopendwa na Bwana, kwa kuwa Mungu amewachagua tangu mwanzo mpate wokofu, katika kutakaswa kwa Roho na kuiamini kweli,
14aliyowaitia ninyi kwa injili yetu, illi kuupata ntukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo.
15Bassi, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ikiwa kwa maneno, au kwa waraka wetu.
16Na Bwana wetu Yesu Kristo, na Mungu Baba yetu aliyetupenda akatupa faraja ya milele na tumaini jema, katika neema,
17awafariji mioyo yenu, na kuwafanya imara katika killa neno na tendo jema.