The chat will start when you send the first message.
1IKAWA huko Ikonio wakaingia pamoja katika sunagogi ia Wayahudi, wakanena; hatta jamaa kubwa ya Wayahudi na ya Wayunani wakaamini.
2Walakini Wayahudi wasioamini wakawataharakisha watu wa mataifa na kuwatia nia mbaya juu ya ndugu.
3Bassi wakakaa huko wakati mwingi, wakinena kwa uthabiti katika Bwana, aliyelishuhudia neno la neema yake, akiwajalia ishara na maajabu yatendeke kwa mikono yao.
4Lakini jamii ya watu wa mjini wakagawanyikana: bawa walikuwa upande wa Wayahudi, na hawa upande wa Mitume.
5Hatta palipotokea shambulio la watu wa mataifa na Wayahudi pamoja na wakubwa wao juu yao, kuwatenda jeuri na kuwapiga mawe,
6bassi, wakapata khabari wakakimbilia miji ya Lukaonia. Lustra na Derbe, na inchi zilizo kando kando:
7wakakaa huko, wakiikhubiri Injili.
8Na huko Lustra palikuwa na mtu mmoja, dhaifu wa miguu, kiwete tangu tumboni mwa mama yake, ambae hajaenda kabisa.
9Mtu huyo alimsikia Paolo akinena; nae akamkazia macho akaona ya kuwa ana imani ya kuponywa,
10akanena kwa sauti kuu, Simama kwa miguu yako sawa sawa. Akasimama upesi akaenda.
11Na makutano walipoona aliyoyafanya Paolo wakapaaza sauti zao, wakisema kwa Kilukaonia, Mungu wametushukia kwa mifano ya wana Adamu.
12Wakamwita Barnaba, Zeu, na Paolo, Herme, kwa sababu ndiye aliyetakadamu katika kimena.
13Kuhani wa Zeu ambae hekalu lake lilikuwa mbele ya mji, akaleta ngʼombe na taji za maua hatta malangoni, akitaka kutoa dhabihu pamoja na makutano.
14Walakini mitume Barnaba na Paolo, walipopata khabari, wakararua nguo zao, wakaenda mbio wakaingia katika makutano, wakipiga kelele, wakisema, Akina hwana, mbona mnafanya haya?
15Sisi nasi tu wana Adamu hali moja na ninyi; twawakhubiri khabari njema mgenke na kuyaacha mambo haya ya ubatili na kumwelekea Mungu aliye hayi, aliyeumba mbingu na inchi na bahari na vitu vyotc vilivyomo:
16ambae zamani zilizopita aliwaacha mataifa yote waende katika njia zao wenyewe.
17Illakini hakujiacha hana shahidi kwa kuwa alitenda mema akiwapeni mvua kutoka mbinguni, na nyakati za mavuno, akiwajaza mioyo yenu chakula na furaha.
18Na kwa maneno haya wakawazuia makutano kwa shidda, wasiwatolee dhabihu.
19Wayahudi wakalika toka Antiokia na Ikonio, wakawashawishi makutano hatta wakampiga mawe Paolo wakamhurura nje ya mji, wakidhani ya kuwa amekwisha kufa.
20Lakini wanafunzi walipokuwa wakimzunguka pande zote, akasimama, akaingia ndani ya mji; na siku ya pili yake akatoka, akaenda zake pamoja na Barnaba hatta Derbe.
21Hatta walipokwisha kuikhubiri Injili katika niji ule, na kupata wanafunzi wengi, wakarejea hatta Lustra na Ikonio na Antiokia,
22wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya shidda nyingi.
23Na walipokwisha kuchagua wazee katika killa mji, na kuomba pamoja na kufunga, wakawaweka kafika mikono ya Bwana waliyemwamini.
24Wakapita kati ya Pisidia wakamgia Pamfulia.
25Na baada ya kukhubiri katika Perga wakatelemka hatta Attalia.
26Na kutoka huko wakasafiri baharini kwenda Antiokia. Huko ndiko walikoombewa neema ya Mungu kwa ile kazi waliyokwisha kuitimiza.
27Hatta walipolika wakalikutanisha Kanisa, wakawaeleza mambo yote aliyoyafanya Mungu pamoja nao, na ya kwaruba amewafungulia mataifa mlango wa imani.
28Wakashinda huko wakati usio mchache, pamoja na wanafunzi.