Matendo 19

Matendo 19

1IKAWA, Apollo alipokuwa Korintho, Paolo, akiisba kupita kati ya inchi za juu, akafika Efeso: akakutana na wanafunzi kadha wa kadba huko:

2akawauliza, Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hatta kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia.

3Akawauliza, Bassi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, Kwa ubatizo wa Yohana.

4Paolo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakaekuja nyuma yake, yaani Kristo Yesu.

5Waliposikia baya wakabatizwa katika jina la Bwana Yesu.

6Na Paolo, alipokwisba kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri.

7Na jumla yao walipata wanaume thenashara.

8Akaingia ndani ya sunagogi, akanena kwa ujasiri, akihujiana na watu kwa muda wa miezi mitatu, na kuwavuta waamini mambo ya ufalme wa Mungu.

9Lakini wengine walikaidi, wakakataa kuamini, wakiitukana ile Njia mbele ya mkutano; bassi, akaondoka akawaacha, akawatenga wanafunzi nao, akahujiana na watu killa siku katika darasa ya mtu mmoja, jina lake Tyranno.

10Mambo haya yakaendelea kwa muda wa miaka miwili, hatta wote waliokaa Asia wakalisikia neno la Bwana, Wayahudi kwa Wayunani.

11Mungu akafanya kwa mikono ya Paolo miujiza ya kupita kawaida;

12hatta wagonjwa wakaletewa leso na nguo zilizogusa mwili wake, magonjwa yao yakawaondokea, pepo wachafu wakawatoka.

13Baadhi ya Wayahudi wenye kutangatanga, nao ni waganga wa pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Twawaapizeni kwa Yesu, yule anaekhubiriwa na Paolo.

14Nao waliofanya haya walikuwa wana saba wa Skewa, Myahudi, kuhani mkuu.

15Yule pepo akawajibu, Yesu namjua na Paolo namfahamu, bali ninyi ni nani?

16Na yule mtu aliyepagawa na pepo akawarukia, akawaweza, akawashinda, hatta wakatoka mbio katika nyumba ile uchi na wamejeruhi.

17Khabari hii ikajulikana na Wayahudi wote na Wayunani waliokaa Efeso, khofu ikawaingia wote, jina la Bwana Yesu likaadhimishwa.

18Na wengi wa wale walioamini wakaja wakaungama, wakidhihirisha matendo yao.

19Na watu wengi katika wale waliotumia mambo ya uganga wakakusanya vitabu vyao, wakavichoma moto mbele ya watu wote: wakafanya hesabu ya thamani yake wakaona ya kwamba yapata fedha khamsini elfu.

20Hivyo neno la Mungu likazidi na kushinda kwa nguvu.

21Mambo hayo yalipokwisha kumalizika, Paolo akaazimu rohoni mwake kupita kati ya Makedonia na Akaia aende Yerusalemi, akisema, Baada ya kuwako huko, yanipasa kuuona na Rumi.

22Akatuma watu wawili miongoni mwa wale waliomkhudumia kwenda Makedonia, nao ni Timotheo na Erasto, yeye mwenyewe akakaa katika Asia kitambo.

23Hatta wakati huo kukatukia ghasia si haba katika khabari ya Njia ile.

24Kwa maana mtu mmoja, jina lake Demetrio, mfua fedha, kazi yake kufanya vihekalu vya fedha vya Artemi, alikuwa akiwapatia mafundi faida nyingi.

25Akawakusanya hao, pamoja na wengine wenye kazi ile ile, akasema, Enyi wanaume, mnajua ya kuwa utajiri wetu hutoka katika kazi hii.

26Tena mnaona na kusikia ya kwamba si katika Efeso tu, bali katika Asia yote pia, Paolo huyo amewaaminisha watu wengi na kuwageuza nia zao, akisema ya kwamba miungu inayofanywa kwa mikono siyo Mungu.

27Si kwamba kazi hii yetu ina khatari ya kudharauliwa, bassi; bali na hekalu ya mungu mke aliye mkuu kuhesabiwa si kitu, na kuondolewa utukufu wake, ambae Asia yote pia na walimwengu wote humwtihudu.

28Waliposikia haya wakajaa hasira, wakapiga kelele, wakisema, Artemi wa Waefeso m mkuu.

29Mji wote ukajaa ghasia, wakaenda mbio wakaingia theatro kwa moyo mmoja, wakiisha kuwakamata Gaio na Aristarko, watu wa Makedonia waliosafiri pamoja na Paolo.

30Na Paolo alipotaka kuingia kati ya watu, wanafunzi hawakumwacha aingie.

31Walakini baadhi ya Waasiarko walio rafiki zake wakatuma watu kwake, wakimsihi asijihudhurishe nafsi yake ndani ya theatro.

32Bassi wengine walikuwa wakilia hivi na wengine hivi: kwa maana ule mkutano umekwisha kuchafukachafuka, na walio wengi hawakuijua sababu ya kukusanyika kwao pamoja.

33Wakatoa Iskander katika mkutano, Wayahudi wakimweka mbele ya watu. Iskander akawapungia mkono, akitaka kuwapa wale watu majibu.

34Lakini walipotambua ya kuwa yeye ni Myahudi, wakapiga kelele wote pia kwa sauti moja kwa muda wa saa mbili au karibu, wakilia, Artemi wa Waefeso ni mkuu.

35Na karani wa mji alipokwisha kuwatuliza watu, akasema, Enyi wanaume wa Efeso, ni mtu gani asiyejua ya kuwa mji wa Efeso ni mtunzaji wa hekalu ya Artemi, mungu mke aliye mkuu, na wa kitu kile kilichoanguka kutoka mbinguni?

36Bassi kwa kuwa mambo haya hayawezi kukanushwa, imewapaseni kutulia, msifanye neno la haraka haraka.

37Kwa maana mmewaleta watu hawa, wasiokwiba vitu vya hekalu wala kumtukana mungu mke wetu.

38Bassi ikiwa Demetrio na mafundi walio pamoja nae wana neno juu ya mtu, baraza ziko, na maliwali wako: na washitakiane.

39Bali mkitafuta neno lo lote katika mambo mengine, yatatengenezwa katika kusanyiko lililo halali.

40Kwa maana tuna khatari ya kushtakiwa fitina kwa ajili ya mambo haya ya leo, ikiwa hakuna sababu ambayo kwa ajili yake tutaweza kujiudhuru kwa mkutano huu.

41Alipokwisba kusema haya akauvunja mkutano.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania