Waebrania 11

Waebrania 11

1BASSI imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.

2Maana kwa hiyo wazee wetu walishuhudiwa.

3Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hatta vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri.

4Kwa imani Habil alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kain; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo ijapokuwa amekufa, angali akinena.

5Kwa imani Enok alihamishwa, asije akaona mauti, wala hakuonekana, kwa sababu Mungu alimhamisha: maana kabla ya kuhamishwa kwake alikuwa ameshuhudiwa kwamba amempendeza Mungu.

6Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu ampendezae Mungu lazima aamini kwamba yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.

7Kwa imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu khabari za mambo yasiyoonekana bado, kwa kumcha Mungu, aliunda safina, apate kuokoa nyumba yake. Kwa hiyo akauhukumu ulimwengu, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani.

8Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, akatoka aende hatta mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako.

9Kwa imani alikaa katika ile inchi ya ahadi, kama katika inchi isiyo yake, akikaa katika khema pamoja na Isaak na Yakobo, warithi pamoja nae wa ahadi ile ile.

10Maana waliutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuujenga na kuufanyiza ni Mungu.

11Kwa imani hatta Sara mwenyewe alipokea nwezo wa kuwa na mimba, alipokuwa amepita wakati wake; kwa kuwa alimwona yeye aliyeahidi kuwa mwaminifu.

12Na kwa ajili ya hayo wakazaliwa na mtu mmoja, nae kama mfu, watu wengi kama nyota za mbinguni wingi wao, na kama mchanga ulio ufukoni, usioweza kuhesabiwa.

13Hawa wote wakafa katika imani, wasizipokee zile ahadi, bali wakiziona tokea mbali na kuzisalimu, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya inchi.

14Maana wasemao maneno kama hayo waonyesha kwa wazi kwamba wanatafuta inchi yao wenyewe.

15Na kama wangaliikumbuka inchi ile waliyotoka, wangalipata nafasi ya kurejea.

16Lakini sasa waitamani inchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea mji.

17Kwa imani Ibrahimu alipojaribiwa, akamtoa Isaak, awe dhabihu; na yeye aliyezipokea ahadi alikuwa akimtoa mwana wake, mzaliwa wake wa pekee;

18naam, yeye aliyeamhiwa, Katika Isaak uzao walio utaitwa,

19akihesabu ya kuwa Mungu aweza kumfufua kutoka kuzimu; akampata tena toka huko kwa mfano.

20Kwa imani Isaak akawahariki Yakobo na Esau, hatta katika khabari ya mambo yatakayokuwa baadae.

21Kwa imani Yakobo, alipokuwa katika kufa, akambariki killa mmoja wa wana wa Yusuf, akaabudu akiegemea kitanda chake.

22Kwa imani Yusuf, alipokuwa amekaribia mwisho wake, alitaja khabari za kutoka kwao wana wa Israeli, akawaagizia mifupa yake.

23Kwa imani Musa, alipozatiwa, akafichwa miezi mitatu na wazazi wake, kwa sababu waliona kwamba ni mtoto mzuri; wala hawakuiogopa amri ya mfalme.

24Kwa imani Musa alipokuwa mtu mzima, akakataa kuitwa mwana wa binti Farao;

25akaona ui afadhali kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha kwa dhambi kitamho;

26akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mwingi kuliko hazina za Misri.

27Kwa imani akatoka Misri, asiogope hasira ya mfalme; maana alistahimili kama amwonae yeye asiyeonekana.

28Kwa imani akaifanya Pasaka, na kunyunyiza ile damu, illi mwenye kuwaangamiza wazaliwa wa kwanza asiwaguse wao.

29Kwa imani wakapita kati ya Bahari ya Sham, kama katika inchi kavu; Wamisri wakaijaribia wakatoswa.

30Kwa imani kuta za Yeriko zikaanguka, zikiisha kuzungukwa siku saba.

31Kwa imani Rahab, yule kahaba, hakuangamia pamoja nao walioasi; kwa kuwa aliwakaribisha wapelelezi kwa amani.

32Na niseme nini tena? Maana wakati usingenitosha kuleta khabari za Gideon na Barak na Samson na Yeftha na Daud na Samwil na manabii;

33ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, waliziba makanwa ya simba,

34walizima nguvu za moto, waliokoka na ukali wa upanga. Walitiwa nguvu baada va kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya wageni.

35Wanawake walipokea wafu wao waliofufuliwa: na wengine walibanwa, wasiukubali ukombozi, wapate ufufuo ulio bora:

36wengine walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa mafungo, na kwa kutiwa gerezani:

37walipigwa mawe, walikatwa kwa msumeno, walishawishwa, waliuawa kwa upanga: walizungukazunguka, wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; waiikuwa wahitaji, wakindhiwa, wakitendwa mabaya:

38(watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao): walikuwa wakizungukazunguka katika nyika na katika milima na katika mapango na katika mashimo ya inchi.

39Na watu hawa wote wakiisha kushuhudiwa kwa sababu ya imani yao, hawakuipokea ahadi:

40kwa kuwa Mungu ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, illi wasikamilishwe pasipo sisi.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania