Yuda 1

Yuda 1

1YUDA, mtumwa wa Yesu Kristo, ndugu wa Yakobo, kwao waliopendwa katika Mungu Baba, na kuhifadhiwa kwa ajili ya Yesu Kristo baada ya kuitwa;

2Rehemana amani na upendano muongezewe.

3Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia khabari ya wokofu wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikieni, illi niwaonye mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu marra moja tu.

4Kwa maana kuna watu wamejiingiza kwa siri, watu walioandikiwa zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufasiki, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo.

5Tena napenda kuwakumbusha, ijapo mmekwisha kujua haya yote, ya kwamba Bwana, baada ya kuwaokoa watu katika inchi ya Misri, aliwaharibu wasioamini.

6Na malaika wasioilinda enzi yao, wakayaacha makao yao, amewaweka kwa hukumu ile kuu katika vifungo vya milele chini ya giza.

7Kama vile bodoma na Gomora, na miji iliyozunguka, waliofuata uasharati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wamepasiwa hukumu yamoto wa milele.

8Kadhalika na hawa, katika kuota kwao, huutia mwili uchafu, hukataa kutawaliwa, hutukana matukufu.

9Lakini Mikael, malaika mkuu, aliposhindana na Shetani, na kuhujiana nae kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana akukemee.

10Lakini watu hawa huyatukana mambo wasiyoyajua, na mambo wayatambuayo kwa asili wajiharibu kwayo kama nyama wasio na akili.

11Ole wao! kwa sababu walikwenda katika njia ya Kain, na kulifuata kosa la Balaam pasipo kujizuia, kwa ajili ya ujira, nao wameangamia katika maasi ya Kora.

12Watu hawa ni miamba yenye khatari katika karamu zenu za upendo wafanyapo karamu pamoja nanyi, wakijilisha pasipo khofu; ni mawingu yasiyo na maji, yachukuliwayo na upepo; ni miti iliyopukutika, isiyo na matunda, iliyokufa marra mbili, na kungʼolewa kabisa;

13ni mawimbi ya bahari vasiyozuilika, yakitoa aibu yao wenyewe kama povu, ni nyota zipoteazo, ambao giza ndio akiba yao waliowekewa milele.

14Na Enok, wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hawo, akisema, Angalia, Bwana alikuja na elfu kumi za watakatifu wake,

15illi afanye hukumu juu ya waiu wote, na kuwaadhibisha wote wasiomcha Mungu, kwa ajili ya kazi zao zote walizoziteuda bila kumcha Mungu, na kwa ajili ya maneno magumu yote ambayo hawo wenye dhambi wasiomcha Mungu wameyanena juu yake.

16Watu hawa ni wenye kunungʼunika, wenye kulalamika, waendao kwa tamaa zao, na vinywa vyao vyanena maneno ya kiburi makuu mno, wakipendelea watu wenye cheo kwa ajili ya faida.

17Bali ninyi, wapenzi, yakumbukeni maneno yaliyonenwa zamani na mitume wa Bwana wetu Yesu Kristo,

18ya kwamba waliwaambia ya kuwa wakati wa mwisho watakuwuko watu wenye kudhihaki, wakizifuata tamaa zao wenyewe zilizo kinyume cha mapenzi ya Mungu.

19Watu hawo ndio wajitengao, watu wa dunia hii tu, wasio na Roho.

20Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imaui yenu iliyo takatifu, na kuomba katika Roho Mtakatifu,

21jilindeni katika upendo wa Mungu, mkingojea rehema ya Bwana wetu Yesu Krislo, hatta mpate uzima wa milele.

22Wahurumiane wengine walio na mashaka;

23bali wengine waokoeni kwa khofu, mkiwanyakua katika moto, mkilichukia hatta vazi lililotiwa takataka na mwili.

24Kwake Yeye awezae kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu,

25Yeye aliye Mungu pekee, mwenye hekima, Mwokozi wetu: kwake yeye utukufu, na ukuu, na uwezo, na nguvu kwa Yesu Kristo, tangu milele, na sasa, na hatta milele. Amin.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania