The chat will start when you send the first message.
1BASSI, ndugu zangu, wapendwa wangu, ninaowaonea shauku, furaha yangu, na taji yangu, simameni imara katika Bwana, wapenzi wangu.
2Namsihi Euodia, namsibi na Suntoke, wawe na nia moja katika Bwana.
3Naam, nakutaka na wewe pia, mjoli wa kweli, uwasaidie wanawake hao; kwa maana waliishindania Injili pamoja nami, na Klementi nae, na wale wengine waliotenda kazi pamoja nami, ambao majina yao yamo katika kitabu cha uzima.
4Furahini katika Bwana siku zote; marra ya pili nasema, Furahini.
5Upole wenu ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu.
6Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika killa neno kwa kusali na kuomba pamoja na kushukuru haja zenu zijulike kwa Mungu.
7Na amani va Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.
8Khatimae, ndugu zangu, mambo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya heshima, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye kuvuma vizuri, ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini haya.
9Mambo mliyojifunza kwangu na kuyapokea, na kuyasikia, na kuyaona kwangu, yatendeni haya; na Mungu wa amani atakuwa pamoja nanyi.
10Nalifurahi sana katika Bwana, kwa kuwa sasa mwisho mmehuisha fikara zenu kwa ajili yangu, kama vile mlivyokuwa mkinifikiri hali yangu; lakini hamkupata nafasi.
11Si kwamba nasema haya kwa kuwa nina mahitaji; maana nimejifunza kuwa radhi na hali yo yote niliyo nayo.
12Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yote, nimefundishwa kushiha na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa.
13Nayaweza mambo yote katika yeye anitiae nguvu.
14Lakini mlifanya vema sana, mkishiriki nami mateso yangu.
15Na ninyi pia, ninyi wenyewe mnajua, enyi Wafilipi, ya kuwa katika mwanzo wa injili, nilipotoka Makedonia, hapana kanisa lingine lililoshirikana nami katika khabari hii ya kutoa na kupokea, illa ninyi peke yenu.
16Kwa kuwa hatta katika Tʼhessaloniki mliniletea msaada kwa mahitaji yangu wala si marra moja tu.
17Si kwamba nakitamani kile kipawa, bali nayatamani mazao yanayozidi kuwa mengi, katika hesabu yenu.
18Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi; tena nimejaa tele, nimepokea kwa mkono ya Epafrodito vitu vile vilivyotoka kwenu, harufu ya manukato, sadaka yenye kibali, impendezayo Mungu.
19Na Mungu atawajazeni killa mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu.
20Sasa Mungu, Baba yetu, atukuzwe milele na milele. Amin.
21Mnisalimie killa mtakatifu katika Kristo Yesu. Ndugu walio pamoja nami wawasalimu.
22Watakatifu wote wawasalimu, khassa wao walio wa nyumba ya Kaisari.
23Neema ya Bwana Yesu Kristo na iwe pamoja na roho zenu. Amin.