The chat will start when you send the first message.
1PAOLO, mtumwa wa Yesu Kristo, aliyeitwa kuwa mtume, na kuwekwa aikhubiri Injili ya Mungu,
2ambayo Mungu amekwisha kuiahidi kwa vinywa vya manabii wake katika maandiko matakatifu,
3khabari za Mwana wake, aliyekuwa katika ukoo wa Daud kwa jinsi ya mwili,
4na kudhihirishwa kwa uweza kuwa Mwana wa Mungu, kwa jinsi ya roho ya utakatifu, kwa ufufuo; Yesu Kristo Bwana wetu,
5ambae katika yeye tulipokea neema na utume illi mataifa yote wapate kujitiisha kwa imani, kwa ajili ya jina lake;
6katika hawa na ninyi mmekuwa, mmeitwa na Yesu Kristo:
7kwa wote walioko Rumi, wapendwao na Mungu, walioitwa kuwa watakatifu: Neema iwe kwenu na imani itokayo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwaua Yesu Kristo.
8Kwanza namshukuru Mungu wangu katika Yesu Kristo kwa ajili yenu nyote, kwa kuwa imani yenu inakhubiriwa katika dunia yote.
9Kwa maana Mungu, nimwabuduye kwa roho yangu katika Injili ya Mwana wake ni shahidi wangu jinsi niwatajavyo pasipo kukoma, siku zote katika sala zangu
10nikiomba nije kwenu sasa katika siku hizi hizi, Mungu akipenda kuifanikisha safari yangu:
11kwa maana ninatamani sana kuwaona, nipate kuwapeni karama ya rohoni, illi mfanywe imara;
12yaani, tufarijiane mimi na ninyi, killa mtu kwa imani ya mwenzake, yenu na yangu.
13Sipendi msiwe na khahari, ndugu zangu, ya kuwa marra nyingi nalikusudia kuja kwemi, nikazuiliwa hatta sasa, illi nipate kuwa na matunda kwenu ninyi pia kama nilivyo navyo katika mataifi mengine.
14Nawiwa na Wayunani na washenzi, nawiwa na wenye hekima na wajinga.
15Kwa hiyo, kwa upande wangu, mimi ni tayari kuikhubiri Injili hatta na kwenu ninyi muaokaa Rumi;
16kwa maana siionci haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokofu, kwa killa aaminiye, kwa Myahudi kwanza, hatta kwa Myunani pia.
17Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake, toka imani hatta imani; kama ilivyoandikwa, Mwenye haki ataishi kwa imani.
18Kwa maana ghadhahu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wana Adamu waipingao kweli kwa uovu wao.
19Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana ni dhahiri ndani yao, kwa maana Mungu aliwadhihirishia.
20Kwa sababu mambo yake yasiyoonekima tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, yanafahamika kwa viumbe vyake, yaani uweza wake wa milele na Uungu wake; wtisiwe na udhuru:
21kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza:
22wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika,
23wakaubadili utukufu wa Mungu asiye ua uharibifu kwa mfano wa sura ya bin-Adamu aliye ua uharibifu, na ya nyama wenye mbawa, na ya nyama wenye miguu mine, na ya nyama watambaao.
24Kwa ajili ya bayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hatta wakavunjiana heshima miili yao:
25kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kwa uwongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anaehimidiwa milele. Amin.
26Kwa hiyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hatta wanawake wakahadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili:
27wanaume vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume kwa wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao.
28Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wuyafanye yasiyowapasa;
29wakijawa na udhalimu wa killa namna ya zina, na novu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na khadaa;
30watu wti nia mbaya, wenye kusengenya, wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakahari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao,
31wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema,
32ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao haya wamestahili mauti, wanafanya haya, wala si hivyotu, bali wakubaliana nao wayatendao.