Tito 2

Tito 2

1BALI wewe nena mambo yapasayo mafundisho ya uzima,

2ya kama wazee wawe wenye kujimudu nafsi zao, wenye adahu, wenye kiasi, wazima katika imani na katika upendo na katika uvumilivu.

3Na wazee wa kike vivyo hivyo wawe na mwenendo wa utakatifu, wasiwe wasiugiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wafundishao mema;

4illi wawatie akili wanawake vijana wawapende wanme zao, ka kuwapenda watoto wao,

5na kuwa wenye niasi, na kuwa safi, kukaa nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao weuyewe, illi neno la Muugu lisitukanwe.

6Na vijana vivyo hivyo nwaonye kuwa na kiasi;

7katika mambo yote ukijionyesha kuwa namna ya matendo mema, katika mafundisho yako ukionyesha usahihi na ustahifu,

8na maneno yenye uzima yasiyoweza kuhukumiwa, illi yule mwenye kupingana nawe ataliayarike, kwa kuwa hana neno baya la kunena juu yetu.

9Watumwa wawatii Bwana zao, wakiwapendeza katika mambo yote; wasiwe wenye kujibu,

10wasiwe waibaji, bali wakionyesha uaminifu mwema wote, illi wayapambe mafundisho ya Mwokozi wetu katika mambo yote.

11Maana neema ya Mungu iwaokoayo wana Adamu wote imeonekana;

12yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia, ua kuishi kwa kiasi, na haki, na utawa, katika ulimwengu wa sasa,

13tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Mungu mkuu, Mwokozi wetu Yesu Kristo;

14aliyejitoa nafsi yake kwa ajili yetu, illi atuokoe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake, walio na juhudi kwa matendo mema.

15Nena maneno hayo, ukaonye ukakaripie kwa mamlaka yote; mtu aliye yote asikudharau.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania