The chat will start when you send the first message.
1Kwanza kabisa, ninakuagiza uwaombee watu wote. Uwaombee kwa Mungu ili awabariki na kuwapa mahitaji yao. Kisha umshukuru Yeye.
2Unapaswa kuwaombea watawala na wote wenye mamlaka. Uwaombee viongozi hawa ili tuweze kuishi maisha yenye utulivu na amani, maisha yaliyojaa utukufu kwa Mungu na yanayostahili heshima.
3Hili ni jambo jema na linampendeza Mungu Mwokozi wetu.
4Mungu anataka kila mtu aokolewe na aielewe kweli kikamilifu.
5Kuna Mungu mmoja tu, na kuna mwanadamu mmoja tu anayeweza kuwaleta pamoja wanadamu wote na Mungu wao. Huyo mtu ni Kristo Yesu kama mwanadamu.
6Alijitoa mwenyewe kulipa deni ili kila mtu awe huru. Huu ni ujumbe ambao Mungu alitupa wakati unofaa.
7Nami nilichaguliwa kama mtume kuwaambia watu ujumbe huo. Ninasema kweli. Sidanganyi. Nilichaguliwa kuwafundisha wasio Wayahudi na nimefanya kazi hii kwa imani na ukweli.
8Nataka wanaume walio kila mahali waombe. Ni lazima wawe watu wanaoishi kwa kumpendeza Mungu na wanaonyoosha mikono yao wanapoomba na wawe watu wasio na hasira na wanaopenda mabishano.
9Na ninawataka wanawake wajipambe kwa namna inayofaa. Mavazi yao yawe yanayofaa na yanayostahili. Hawapaswi kuvutia watu kwa kutengeneza nywele zao kwa mitindo ya ajabu ama kwa kuvaa dhahabu, vito au lulu au nguo za gharama.
10Lakini wajipambe na kuvutia kwa matendo mema wanayofanya. Hayo ndiyo yanayofaa zaidi kwa wanawake wanaosema kuwa wamejitoa kwa ajili ya Mungu.
11Mwanamke anapaswa kujifunza akisikiliza kwa utulivu huku akiwa radhi kutii kwa moyo wake wote.
12Simruhusu mwanamke kumfundisha mwanaume au kumwelekeza jambo la kufanya. Bali lazima asikilize kwa utulivu,
13kwa sababu Adamu aliumbwa kwanza na Hawa akaumbwa baadaye.
14Na Adamu hakudanganywa. Bali mwanamke ndiye aliyedanganywa naye akatenda dhambi.[#2:14 “Adamu siye aliyedanganywa” Shetani alimdanganya Hawa, naye Hawa alisababisha Adamu kutenda dhambi. Tazama Mwa 3:1-13.]
15Lakini wanawake wataokolewa kwa jukumu lao la kuzaa watoto. Wakiendelea kuishi katika imani, upendo, utakatifu na tabia njema.[#2:15 Kwa maana ya kawaida, “Ataokolewa katika kazi yake ya kuzaa watoto.” Kuzaa watoto, inaweza kutumika hapa kama kielelezo cha maana ya “kuzaa sifa njema”, zinazofafanuliwa katika mstari unaofuata.]