The chat will start when you send the first message.
1“Kama Mwenyezi-Mungu asingalikuwa upande wetu
Semeni nyote mlio katika Israeli:
2“Kama Mwenyezi-Mungu asingalikuwa upande wetu,
wakati ule tuliposhambuliwa na maadui,
3hakika tungalimezwa tukiwa hai,
wakati hasira zao zilipotuwakia.
4Tungalikumbwa na gharika,
tungalifunikwa na mto wa maji,
5mkondo wa maji ungalituchukua!”
6Atukuzwe Mwenyezi-Mungu,
ambaye hakutuacha makuchani mwao.
7Tumeponyoka kama ndege mtegoni;
mtego umeteguliwa, nasi tukaokoka.
8Msaada wetu watoka kwa Mwenyezi-Mungu,
aliyeumba mbingu na dunia.