Zaburi 129

Zaburi 129

Sala dhidi ya maadui wa Israeli

1“Nimesumbuliwa vibaya tangu ujana wangu

Kila mtu katika Israeli na aseme:

2“Nimesumbuliwa vibaya tangu ujana wangu,

lakini hawakufaulu kunishinda.

3Walinijeruhi vibaya mgongoni mwangu,

wakafanya kama mkulima anayelima shamba.

4Lakini Mwenyezi-Mungu ni mwadilifu;

amezikata kamba za hao watu waovu.”

5Na waaibishwe na kurudishwa nyuma,

wote wale wanaouchukia mji wa Siyoni.

6Wawe kama nyasi juu ya paa la nyumba,

ambazo hunyauka kabla hazijakua,

7hakuna anayejishughulisha kuzikusanya,

wala kuzichukua kama matita.

8Hakuna apitaye karibu atakayewaambia:

“Mwenyezi-Mungu awabariki!

Twawabariki kwa jina la Mwenyezi-Mungu!”

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote (Yenye Vitabu vya Deuterokanoni): Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa (BHN): Hakimiliki -1995, 2001: kwa Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Published by: Bible Society of Tanzania