The chat will start when you send the first message.
1Ni jambo zuri na la kupendeza sana
ndugu kuishi pamoja kwa umoja.
2Ni kama mafuta mazuri yatiririkayo kichwani,
mpaka kwenye ndevu zake Aroni,
mpaka upindoni mwa vazi lake shingoni.
3Ni kama umande wa mlima Hermoni,
uangukao juu ya vilima vya Siyoni!
Huko Mwenyezi-Mungu ameahidi kuwabariki watu wake,
kuwapa uhai usio na mwisho.