Zaburi 121

Zaburi 121

Mungu kinga yetu

1Natazama juu milimani;

msaada wangu utatoka wapi?

2Msaada wangu watoka kwa Mwenyezi-Mungu,

aliyeumba mbingu na dunia.

3Hatakuacha uanguke;

mlinzi wako hasinzii.

4Kweli mlinzi wa Israeli

hasinzii wala halali.

5Mwenyezi-Mungu ni mlinzi wako;

yuko upande wako wa kulia kukukinga.

6Mchana jua halitakuumiza,

wala mwezi wakati wa usiku.

7Mwenyezi-Mungu atakukinga na baya lolote;

atayalinda salama maisha yako.

8Mwenyezi-Mungu atakulinda katika shughuli zako zote[#121:8 Kiebrania neno kwa neno ni “uingiapo na utokapo” fungu la maneno lenye maana ya matendo ya mtu kwa jumla.]

tangu sasa na hata milele.

Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993 The Bible Society of Kenya 1993
Published by: Bible Society of Tanzania