The chat will start when you send the first message.
1Nilifurahi waliponiambia:
“Twende nyumbani kwa Mwenyezi-Mungu.”
2Sasa tuko tumesimama,
kwenye malango yako, ee Yerusalemu!
3Yerusalemu, mji uliojengwa,
ili jumuiya ikutane humo.
4Humo ndimo makabila yanamofika,
naam, makabila ya Israeli,
kumshukuru Mwenyezi-Mungu kama alivyoagiza.
5Humo mmewekwa mahakama ya hukumu ya haki,
mahakama ya ukoo wa kifalme wa Daudi.
6Uombeeni Yerusalemu amani:
“Wote wakupendao na wafanikiwe!
7Ndani ya kuta zako kuwe na amani,
majumbani mwako kuweko usalama!”
8Kwa ajili ya jamaa na ndugu zangu,[#122:8 Hawa ni Waisraeli wenzi wa huyo Mwanazaburi ambao waliishi huko Yerusalemu.]
ee Yerusalemu, nakutakia amani!
9Kwa ajili ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu,
ninakuombea upate fanaka!