The chat will start when you send the first message.
1Pendeni haki, enyi watawala wa dunia![#1:1 Hapa ni sawa na kuishi kulingana na matakwa ya Mungu, kufuata maagizo yake, hasa yale ya kuwatendea wengine kwa haki. Katika sehemu yote hii ya kwanza, haki inabainishwa na kuwekwa kinyume cha uovu na ni wazo muhimu.; #1:1 Mwandishi anaongea kana kwamba angekuwa yeye ni mfalme Solomoni ambaye anaweza kuwaambia hao watawala kwa mamlaka. Maagizo anayowapa yanahusu hasa kuiongoza jumuiya.]
Jiaminisheni kikamilifu kwa Bwana.
na kumtafuta kwa moyo mnyofu.
2Maana yeye huwajalia wanaojiaminisha kwake wampate;
hujionesha kwa wale wanaomtegemea.
3Fikira potovu huwatenganisha watu mbali na Mungu;
watu wakiijaribu nguvu yake, yeye hudhihirisha upumbavu wao.
4Hekima haiingii kwa mtu mdanganyifu,[#1:4 Wazo hili ndilo kiini cha ujumbe wa kitabu chote (taz Utangulizi). Tofauti na hekima ya kibinadamu hii ina chanzo chake kwa Mungu na inahitaji hali au mazingira ya uadilifu ili mtu aweze kuipokea. Inaelezwa kinaganaga zaidi katika sehemu ya pili ya kitabu hiki (6:1—9:18).]
wala haikai kwa mtu aliye mtumwa wa dhambi.
5Mtu aliye mtakatifu amejifunza kuepukana na udanganyifu.
Mtu huyo huepa kushiriki fikira za kipumbavu;
huwa na wasiwasi endapo haki zinavunjwa ovyo.
6Hekima ana moyo wa huruma;
lakini hatamsamehe yeyote anayemkufuru Mungu.
Mungu ajua yote: hisia zetu na fikira zetu;
husikia kila neno tusemalo.
7Roho ya Bwana inaujaza ulimwengu;
hiyo inayotegemeza kila kitu pamoja.
hujua kila kitu asemacho binadamu.
8Kila mtu asemaye mabaya dhidi yake hawezi kufichika,
na hukumu inapotolewa hataweza kuiepa adhabu.
9Mawazo ya waovu yatachunguzwa;
Bwana atapata ripoti ya maneno yao mabaya
na kuwaadhibu kwa sababu ya uovu wao.
10Bwana ametega sikio lake; anasikia kila kitu.
Hakuna mnong'ono wowote ule ambao utasitirika.
11Kwa hiyo jihadharini na manung'uniko ya bure,
epukeni kusema uchongezi.
Mungu husikia hata nung'uniko la siri kabisa.
Asemaye uongo huiangamiza roho yake mwenyewe.
12Kwa hiyo usijiletee kifo kwa dhambi zako,
wala kukaribisha maangamizi kwa matendo yako maovu.
13Kifo hakikuanzishwa na Mungu;[#1:13 Rejea 2:23-24.]
Mungu hafurahii kufa kwa mtu yeyote yule.
14Mungu aliumba viumbe vyote vipate kuwapo,
akavipa nguvu zifaazo za kuendeleza maisha.
Ndani ya viumbe hamna sumu ya kuua;
Kuzimu haina mamlaka hapa duniani.
15Mwadilifu ataishi milele![#1:15 Wazo kuhusu kuishi daima baada ya kifo linapatana na matazamio makubwa ya wasomaji ambao walijua utamaduni wa Kigiriki kuhusu Mungu (rejea 3:1-4).]
16Lakini wasiomcha Mungu hukaribisha kifo kwa matendo na maneno yao,[#1:16 Katika sehemu hii mwandishi anazingatia kueleza namna ya kufikiri na kuishi kwa hao waovu. Rejea 2:21-22; 3:10.]
hufanya urafiki na kifo
na kufanya mkataba pamoja nacho;
sasa wanastahili kuwa mateka wake!